The House of Favourite Newspapers

Yanga wapeni furaha Watanzania

0

Majimaji Vs Yanga (14)
WAWAKILISHI wa Tanzania kwenye michuano ya kimataifa katika ngazi ya klabu, Yanga kesho Jumanne watakuwa Uwanja wa Taifa jijini Dar wakivaana na TP Mazembe ukiwa ni mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika. Yanga ilianza vibaya mchezo wao wa kwanza kwani ilipoteza mbele ya wenyeji Mo Bejaia ya Algeria kwa bao 1-0 lakini hiyo itakuwa imewapa morali zaidi ya kuhakikisha mchezo wa kesho wanashinda.

Watanzania kwa pamoja ni vizuri tukaungana na Yanga kwenda kuwapa sapoti pale Taifa kwani wao wanaiwakilisha nchi kimataifa hivyo tuachane na mambo ya ushabiki wa utani wa jadi kwani hata wageni watatushangaa kama wakiona tumeungana nao kuwapa sapoti na kuwaacha wawakilishi wetu.

Lakini pia kwa wachezaji mnatakiwa mcheze kwa kujituma na kuhakikisha ushindi unapatikana ili kujiweka katika nafasi nzuri kwenye msimamo wa kundi lenu. Ushindi wowote mtakaoupata utakuwa na maana kubwa kwani ni vyema mkautumia uwanja wa nyumbani vizuri na ugenini iwe ni kutafuta sare au ushindi kwa kila iwezekanavyo.

Leave A Reply