×

Jerry Muro Atemwa Yanga

PHILLIP NKIN | CHAMPIONI, Dar es Salaam

UNAWEZA kusema kweli hali ya uchumi ni ngumu na Klabu ya Yanga, ime­amua kupitisha “fagio la chu­ma” ili kufanya punguzo la wafanyakazi wake kwa lengo la kuweza kuende­lea kujiendesha.

Kati ya wanaoon­doka katika orodha ya watumishi wa Yanga ni Mkurugenzi wa Habari wa klabu hiyo, Jerry Cor­nel Muro ambaye ame­kuwa akiendesha kipindi cha runinga katika runinga ya ITV na uchambuzi katika Gazeti la Namba Moja la Michezo nchini la Cham­pioni.

Mkataba wa Yanga na Muro umemalizika Desemba, mwaka jana. Tangu hapo, Yan­ga haikuwa imemuongezea mkataba. Na imeonekana ana­paswa kuingia kwenye orodha hiyo kwa kuwa kati ya wale wasio na mchango mkubwa kwa sasa.

Jerry Muro na Manara

Muro amefungiwa mwaka mmoja na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), hivyo amekuwa hazungumzi lol­ote kuhusiana na Yanga.

Taarifa kutoka ndani ya kamati ya utendaji zimeeleza kuwa, Katibu Mkuu mpya wa Yanga, Charles Boniface Mk­wasa ndiye atakayetoa taarifa kwa wafanyakazi kumi na moja ambao wamekum­bwa na “fagio la chuma”.

Mmoja wa wajumbe wa kamati ya utendaji ya Yanga, amesema uongozi tayari umewasiliana nao na wameridhia Jerry aondoke.

“Kweli na ninakuhakikishia, uamuzi wa uongozi ni kubana matumizi zaidi. Hivyo tunachokifanya hapa kwa pamoja kama­ti ya utendaji na uongozi ni kuangalia hali ilivyo,” kilieleza chanzo hicho.

“Unajua Yanga inakwenda kwa hasara, mechi kuonyeshwa kwenye Azam TV ni tatizo kubwa kabisa. Hakuna tunachopata na sasa imefikia tunashindwa kulipa mishahara. Wako ambao wanajikaza hawasemi ukweli, lakini siku itafika tu hawatavumilia haya maumivu.

“Najua suala la Muro litawashitua watu wengi lakini ni mtu mwenye kazi yake kwa kuwa ni mtaalamu wa masuala ya habari. Kila mjumbe wa kamati anajua na hii ni kwa ajili ya nia njema kwa klabu na wote tumeridhia.

“Tunafanya hivi ili kuweza kuende­lea kuwalipa wachezaji na wafanyaka­zi wengine. Ingekuwa mambo ni ma­zuri, hakuna ambaye angeondolewa.”

Pamoja na Muro, “panga” hilo limepita kwenye vitengo vya fedha, masoko, usafi na ulinzi.

Mmoja wa waliokumbwa na “pan­ga” hilo ni bwana fedha, Faidhal Mike ambaye nafasi yake inachukuliwa na Baraka Deusdedit aliyekuwa kaimu katibu mkuu wa Yanga kwa kuwa nafasi hiyo imempata mwenyewe ambaye ni Charles Boniface Mkwasa aliyetangazwa rasmi jana na Maka­mu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga.

Ikumbukwe kwamba pamoja na ushabiki wa Simba na Yanga, lakini mashabiki wa timu zote walikuwa wakifurahishwa sana na kauli za msemaji huyo, hasa wakati mechi ya Simba na Yanga ikiwa inakaribia.

Pamoja na upinzani wao, lakini Muro ni rafiki mkubwa wa ‘nje ya uwanja’ na Haji Manara ambaye ni mse­maji wa klabu ya Simba.

 

Save

Save

Save

Save

Shinda Nyumba Awamu ya Pili Yatikisa Jiji la Dar es Salaam