Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa akitoa mawaidha mbele ya waumini wa kiislamu katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu Majaliwa akiendelea kutoa mawaidha yake kwa waumini hao ambao hawapo pichani.
Mufti Mkuu wa Tanzania, Shekh Abubakar Zubery akitoa mawaidha yake mbele ya waumini wa kiislamu.
Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhadi Mussa akiongea na waumini wa dini hiyo na kuwatakia sikukuu njema waislamu wote nchini.
Kutoka kushoto mbele ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi, Rais Mstaafu, Ally Hassan Mwinyi na Waziri Mkuu, Kassimu Majaliwa.
Alhadi Mussa akihutubia waumini wa dini ya kiislamu katika Viwanja vya Mnazi Mmoja.
Taswira ya baadhi ya waumini waliojitokeza katika Viwanja vya Mnazi Mmoja inavyoonekana.
Sehemu ya waumini akinamama walijitokeza katika swala hiyo kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja.
WAZIRI Mkuu wa Tanzania, Majaliwa Kassim Majaliwa mapema leo Jumatano, ameongoza waumini wa dini ya kiislamu katika swala ya Eid El Fitr iliyofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waumini mara baada ya swala hiyo, Waziri Mkuu Majaliwa aliwataka waislamu wote nchini kusherehekea sikukuu hiyo kwa kufanya matendo mema ya kumpendeza Mwenyezi Mungu.
Amewataka waumini wote kuwaombea dua maalum watu waliopoteza maisha katika ajali ya gari iliyopoteza maisha ya abiria 30 iliyotokea juzi Jumatatu mkoani Singida.
Naye Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakary Zubery amewaomba waumini wa dini hiyo na wakristo kukaa pamoja na kula pamoja, kusherehekea sikukuu hiyo ikiwemo kutoa sadaka kwa wagonjwa na wasiojiweza.
Aidha Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhadi Mussa Salum naye alitoa nasaha zake kwa waumini wote wa kiislamu kwa kufikisha siku ya leo ya mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani na kuwataka wanaoendelea kwa kufunga sita wawe na mfungo mwema.
NA DENIS MTIMA/GPL





