Mratibu wa Baraza la Usimamizi wa Mazingira Kanda ya Mashariki (NEMC), Jaffar Chimgege, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani), Dar es Salaam, Kulia ni Ofisa mazingira mwandamizi wa baraza hilo, Aziz Abbu (Picha na Maktaba).
Baraza la Taifa la Usimamizi na Hifadhi ya Mazingira NEMC limefunga kiwanda cha unga na nafaka cha Twenty First (21) Centuary kilichopo Sinza Jijini Dar es Salaam sambamba na kukitoza faini ya shilingi milioni 35.
Baraza hilo limefikia maamuzi hayo sababu kiwanda hicho kimejiendesha kwa zaidi ya miaka kumi sasa bila kuwa na Cheti cha Tathmini ya Athari ya Mazingira ambalo ni kinyume cha sheria za nchi huku kikimwaga vumbi kali kwenye makazi ya watu.