×

Yemi Alade amuomba ferarri rais

Yemi-Alade-AFWN-BellaNaija-10-600x400  Lagos, Nigeria

BAADA ya kutinga na gauni la milioni 15 katika siku ya utoaji tuzo za BET 2016 na kutengeneza vichwa vya habari, staa wa muziki kutoka Nigeria, Yemi Alade ameweka tena vichwa vya habari baada ya kuibuka na kumuomba ‘kiaina’ Rais wa Togo, Faure Gnassingbé gari aina ya Ferrari.

Yemi-Alade-Staa huyo anayebamba na Ngoma ya Ferrari, kupitia ukurasa wake wa Instagram alitupia picha ikimuonesha akipeana mkono na rais huyo kisha akaandika;

“Haihitaji chujio kujua nipo na Rais wa Togo, Faure (pichani). Asante sana mheshimiwa na nasubiri Ferrari langu.”

Yemi-AladeKutokana na ujumbe huo, mashabiki wake wengi wamekuwa na mawazo tofauti huku wengine wakifikiri kuwa ameahidiwa kupewa mkoko huo.

 

Leave a Comment