×

Shigongo Awahimiza Wanafunzi Kujiongezea Vipato

5

Mwenyekiti wa Muhimbili University Fellowship of Evangelical Students (MUFES), Joseph Asenga,  akimkaribisha Mkurugenzi wa Global Publishers, Eric  Shigongo (kulia).

8

10

Shigongo akihutubia wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Udaktari Muhimbili ambao wameunda umoja wao unaojulikana kama Muhimbili University Fellowship of Evangelical Students.

11

Wanafunzi hao wakiendelea kumsikiliza.

13

…Wakimpigia makofi Shigongo (hayupo pichani).

Capture

Shigongo akisalimiana na baadhi ya wanafunzi wa MUFES baada ya kuwasili chuoni hapo kuwahutubia.

MKURUGENZI Mtendaji wa Kampuni ya Global Publishers, Eric Shigongo, jsns  Jumamosi  alihutubia wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Udaktari Muhimbili ambao wameunda umoja wao unaojulikana kama Muhimbili University Fellowship of Evangelical Stdents  (MUFES) na kusema kuwa taaluma wanayoichukua ni nzuri lakini akawashauri kujiongezea vipaji vingine ili kujiongozea mapato.
Shigongo ambaye alikuwa mgeni rasmi katika kikundi hicho ambacho kilifanya mkutano wake katika ukumbi uliopo chuoni hapo ujulikanao kwa jina la Muhimbili Lecture Theatre 5, aliwahimiza wanachuo hao kuwa na ubunifu mkubwa ili kuweza kufanikiwa katika maisha.
“Wito wangu ni kwamba muwe na vyanzo vingi vya mapato katika maisha yenu kwani kuwa na vyanzo vingi vya mapato kutawafanya mjiongezee nafasi kubwa ya kukuza uchumi na kuleta maendeleo ndani ya familia zenu,” alisema Shigongo.
Pia aliwahimiza wanafunzi hao kutokata tamaa katika maisha yao hata kama watakuwa wanakutana na vikwazo vingi kwani hayo ni madaraja tu ya mapito ili waweze kufanikiwa.

(HABARI: Hilaly Daudi, Global TV Online/GPL)

Leave a Comment