HIVI sasa kele za usajili zimepamba moto barani Ulaya. Mchuano ni mkali, kila kocha anataka kuimarisha kikosi chake. Championi Jumatatu kwa msaada mkubwa wa mtandao, linakuletea dili ambazo zilikamilika wiki iliyopita na nyingine zinakaribia kabisa kukamilika huku zikiwa zimebaki wiki sita tu kabla ya dirisha la usajili kufungwa mwishoni mwa Agosti:
GOMIS ANAKWENDA UFARANSA
Bafetimbi Gomis yupo njiani kuelekea Ufaransa. Straika huyo Mfaransa aliifungia Swansea mabao saba msimu uliopita lakini yupo huru kuondoka. Ameachwa kwenye kikosi kilichokwenda Marekani kujiandaa na msimu mpya na yupo karibu kutua Marseille kwa mkopo.
JORDON IBE ATUA BOURNEMOUTH
Winga huyo ameiacha Liverpool kwa dau la pauni milioni 15, Ijumaa iliyopita.
KANTE HUYOO CHELSEA
N’Golo Kante yupo karibu kabisa kutangazwa kama mchezaji mpya wa Chelsea akitokea Leicester. Kante amekubali kusaini mkataba wa miaka mitano kwa dau la pauni milioni 30.
MORENO ATUA KWA GUARDIOLA
Manchester City ambayo hivi sasa ipo chini ya kocha Pep Guardiola, imekamilisha usajili wa nyota kinda wa Colombia, Marlos Moreno. Fowadi huyo, 19, ametokea Klabu ya Atletico Nacional ya nchini kwao na inasemekana ni moto kwelikweli. Amenaswa kwa dau la pauni milioni 8.23.
MATIP RASMI LIVERPOOL
Beki kisiki Joel Matip amenaswa na mikono ya Jurgen Klopp katika kikosi cha Liverpool. Mcameroon huyo, 24, amejiunga na kikosi hicho kama mchezaji huru akitokea Schalke ambayo ameitumikia kwa miaka 16.
ROMA YAMNASA JESUS
AS Roma imethibitisha kumsajili beki Juan Jesus kutoka Inter Milan. Ametua kwa mkopo mrefu wa msimu wa dau la pauni mil 1.7.
KLUIVERT AULA PSG
Fowadi wa zamani wa Ajax, Barcelona na Newcastle, Patrick Kluivert raia wa Uholanzi, ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Soka wa Klabu ya PSG ya Ufaransa.
SUBOTIC ATUA MIDDLES-BROUGH
Middlesbrough wamemnasa beki wa kati Mserbia, Neven Subotic kutoka Borussia Dortmund. Amesaini mkataba wa miaka mitatu kwa dau linalosemekana kuwa ni pauni milioni nane.
NEGREDO ATUA MIDDLESBROUGH KWA MKOPO
Middlesbrough imekubaliana na Valencia kumchukua Alvaro Negredo kwa mkopo. Straika huyo wa zamani wa Man City, alitarajiwa kupata vipimo vya afya wikiendi iliyopita. Valencia imemuondoa baada ya kumpata Mreno, Luis Nani. Negredo aliwahi kuifungia City mabao 23 katika michezo 48 kwa msimu kabla ya kuondoka kikosini hapo.
GIACCHERINI ATUA NAPOLI
Kiungo mshambuliaji aliyeng’ara kwenye Euro 2016 akiwa na Italia, Emmanuele Giaccherini, 31, amekamilisha usajili wake katika kikosi cha Napoli akitokea Sunderland ambayo msimu uliopita ilimtoa kwa mkopo katika kikosi cha Bologna.
SKRTEL AJIUNGA FENERBAHCE
Usajili wa beki wa Liverpool, Martin Skrtel katika kikosi cha Fenerbahce umeshathibitishwa.
Raia huyo wa Slovakia alifanyiwa vipimo wiki iliyopita na kuhitimisha miaka yake nane katika kikosi cha Liver. Amenaswa kwa dau la pauni mil 5.5.
DIGNE ATUA BARCELONA
Liverpool ilitupa ndoano kwa beki wa kushoto Mfaransa, Lucas Digne, kabla ya kuitosa ofa hiyo na mahaba yake kuyaelekeza Barcelona ambayo imemnasa kwa dau la pauni mil 16.7. Msimu uliopita, alikuwa akiichezea Roma kwa mkopo akitokea PSG.
BENATIA ASAINI JUVENTUS
Juventus imekamilisha usajili wa beki Mmorocco, Medhi Benatia kutoka Bayern Munich. Nyota huyo, 29, alishindwa kupata nafasi ya kutosha Bayern ambayo aliichezea tangu 2014 tu. Kutua kwake kunaweza kumfanya Leonardo Bonucci aende Manchester City.
MAN CITY YAMNASA SANE
Manchester City imekamilisha usajili wa kiungo mpambanaji Leroy Sane kutoka katika kikosi cha Schalke. City imempa kiungo huyo mshambuliaji ofa ya mkataba wa miaka minne kwa dau la pauni milioni 42. City inamchukulia Sane kama kinda atakayekuja kuitikisa dunia hivi karibuni. Msimu uliopita alifunga mabao tisa na kutoa pasi za mabao saba.
WACHEZAJI WENGINE AMBAO WAMESHASAJILIWA (ENGLAND TU)
Arsenal:
Granit Xhaka – Gladbach, pauni 34m
Takuma Asano – Hiroshima, imefichwa
Burnley:
Jamie Thomas – Bolton, huru
Robbie Leitch – Motherwell, huru
Bournemouth:
Lys Mousset – Le Havre, pauni 5.4m
Emerson Hyndman – Fulham, pauni 0.75m
Nathan Ake – Chelsea, mkopo
Lewis Cook – Leeds, pauni 10m
Chelsea:
Michy Batshuayi – Marseille, pauni 33.2m
Crystal Palace:
Andros Townsend – Newcastle United, pauni 13m
Steve Mandanda – Marseille, huru
James Tomkins – West Ham, pauni 10m
Everton:
Maarten Stekelenburg – Fulham, imefichwa
Bassala Sambou – Coventry, kufidia
Chris Renshaw – Oldham, imefichwa
Hull:
Jonathan Edwards – Peterborough, huru
Will Mannion – Wimbledon, kufidia
Leicester:
Nampalys Mendy – Nice, pauni 13m
Ron-Robert Zieler – Hannover 96, pauni 2.6m
Luis Hernandez – Sporting Gijon, huru
Raul Uche Rubio – Rayo Vallecano, imefichwa
Ahmed Musa – CSKA Moscow, imefichwa
Liverpool:
Sadio Mane – Southampton, pauni 36m
Loris Karius – Mainz, pauni 4.7m
Joel Matip – Schalke, huru
Man City:
Ilkay Gundogan – Dortmund, pauni 21m
Nolito, Celta Vigo, pauni 13.8m
Oleksandr Zinchenko – FK Ufa, imefichwa
Aaron Mooy – Melbourne City, huru
Man United:
Zlatan Ibrahimovic
Eric Bailly – Villarreal, pauni 30m
Henrikh Mkhitaryan – Dortmund, pauni 26.3m
Middlesbrough:
Marten de Roon – Atalanta, pauni 12m
Viktor Fischer – Ajax, pauni 3.8m
Bernardo Espinosa – Sporting Gijon, huru
Jordan McGhee – Hearts, mkopo
Victor Valdes – huru
Southampton:
Nathan Redmond – Norwich, pauni 11m
Pierre-Emile Hojbjerg – Bayern Munich, imefichwa
Stoke City:
Hawajatangaza
Sunderland:
Hawajatangaza
Swansea:
Leroy Fer – QPR, pauni 4.75m
Mike van der Hoorn – Ajax, imefichwa
Tyler Reid – Manchester United, imefichwa
George Byers – Watford, huru
Tottenham:
Vincent Janssen – AZ Alkmaar, pauni 18.6m
Victor Wanyama – Southampton, pauni 11m
Watford:
Isaac Success – Granada, pauni 12.5m
Christian Kabasele – Genk, pauni 5.8m
Jerome Sinclair – Liverpool, huru
Juan Camilo Zuniga – Napoli, mkopo
West Brom:
Matt Phillips – QPR, pauni 5.5m
West Ham:
Manuel Lanzini – Al Jazira Club, pauni 9.4m
Toni Martinez – Valencia, pauni 2.25m
Havard Nordtveit – Gladbach, huru
Sofiane Feghouli – Valencia, huru
Gokhan Tore, Besiktas, mkopo
Domingos Quina – Chelsea, huru
Ashley Fletcher – Man United, huru.
