
Jeneza la marehemu Sajent Alex Njau aliyeuawa usiku wa Ijumaa wiki iliyopita kwa kupigwa risasi.
ASKARI wa usalama barabarani Sajent Alex Njau aliyeuawa usiku wa Ijumaa wiki iliyopita kwa kupigwa risasi mbili kifuani na watu ambao hawajajulikana wakati akiwa kazini, mwili wake umeagwa leo nyumbani kwake maeneo ya Kunduchi jijini Dar es Salaam na kuanza safari ya kuelekea mkoani kwao Moshi, Mamba-Marangu kwa mazishi.
Katika tukio hilo, Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu, Simon Sirro, amesema jeshi litapambana kwa hali na mali kuhakikisha waliohusika na tukio hilo wanachukuliwa hatua kali za kisheria.
“Nataka niiambie familia ya marehemu kwamba msiba huu umetusikitisha sana na niwaahidi kwamba tutafanya juu chini kuhakikisha wahusika wote waliohusika wanapatikana na wanashughulikiwa ipasavyo kisheria. Lazima wahusika tuwapate wakiwa hai au wamekufa, hata kama aliyehusika yupo ndani ya familia tutamgonga tu,” alisema.

Ndugu wa marehemu akibebwa baada ya kupoteza fahamu.

Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Kinondoni, Awadhi J. Haji, akitoa neno.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum, Simon Sirro akizungumza machache msibani.

Mbunge wa zamani wa Kinondoni, Iddi Azan, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama Barabarani Mkoa wa Kinondoni akieleza machache msibani hapo.

…Akitoa salamu za mwisho.

Kamanda wa Polisi Kinondoni, Christopher Fuime (wa pili kushoto) akiaga mwili wa marehemu.

Baadhi ya matrafiki wakiaga wakitoa heshima zao za mwisho kwa marehemu.

Baadhi ya polisi wakimuaga marehemu.

Jeneza likipakizwa garini tayari kwa safari ya kwenda Moshi.
Na Mayasa Mariwata/GPL