×

Bila bilioni 100 watanzania waliowekwa bond Ughaibuni hawaachiwi

AtekwaWAANDISHI WETU, Amani

DAR ES SALAAM: Mtanzania Adam Akida, mkazi wa Magomeni-Mapipa anayedaiwa kuwekwa rehani (bond) nchini Pakistan na Wabongo wengine kadhaa ambao nao wako katika hali hiyo kwenye nchi mbalimbali duniani, huenda wakauawa endapo kiasi cha shilingi bilioni 100 hazitapatikana ili kuwakomboa, Amani inakujuza.

Kwa kujibu wa chanzo cha kipolisi, Adam si Mtanzania wa kwanza kukumbwa na kibano cha rehani nchini Pakistan kwani wapo Wabongo wengine nchini humo ambao wanashikiliwa na wauza waunga baada ya wenzao kuwaweka dhamana bila kurejea na pesa za watu.

SIKIA HABARI HII

“Mimi nawapa habari, lakini ni kutokana na hili sakata la Mtanzania Adam Akida kuwekwa rehani nchini Pakistan. Ni kweli atakuwa anateswa sana kule kwa tabia ya watu wanaowapokea watu wa rehani.

“Lakini sasa unajua ishu hizi si za kiserikali. Ni makundi ya wachache ambao wanafanya biashara haramu kwa kujificha. Kuna Watanzania wengi sana, kama hamsini wapo nje ya nchi wamewekwa bond.”

NCHI ZATAJWA

 “Nchi ambazo Wabongo wapo ni Pakistan, Brazil, Iran, Sauz (Afrika Kusini), Uturuki na Venezuela. Wabongo wengi walijiingiza kwenye biashara hiyo huko na kujikuta wakiwa kwenye kibano au mikono ya Wazungu wa unga (wauza unga wakubwa).”

MAJINA HAYA

“Kwa leo hapa nayakaumbuka majina machache sana. Kuna Jumanne Ismail (Pakistan), Hamis Mohamed (Brazil), Juma Jumadin (Brazil), Isaya Masha (Iran), Michael Adam (Sauz) na Mohamed Abdul (Sauz).

“Wengine ni Faiz (Sauz), Jordan Lau (Brazil) na Mkarama ‘Mintu’ Hassan (Pakistan). Hayo ndiyo majina naweza kuyakumbuka hapa kwenye karatasi yangu ya rafu! Hawa wote tuna habari zao za kiinte-lijensia kwamba wamewe-kwa bond.

“Sasa tofauti hapa ni moja tu, kwamba wengi wapo wana-subiri kukomb-olewa. Tulipo-fuatilia kwa kina wote hamsini zinata-kiwa kama bilioni mia moja hivi, kama hazijapatikana wapo hatarini, wanaweza kuuawa.”

KUHUSU KUTESWA

“Unajua, kama mliona video ya Adam akiteswa, wapo ambao huko walipo hawateswi, wamekaa tu kama dhamana, jamaa wanasubiri chao wawaachie, sasa wanavyochelewa ndipo hatari hujitokeza,” kiliongeza chanzo.

JESHI LA POLISI BONGO

“Kifupi, Jeshi la Polisi Tanzania halina cha kufanya kwa sababu hao watu waliondoka wenyewe, tena wengi waliaga makwao kwamba wanakwenda kufanya biashara lakini hawakusema ni biashara gani.

“Pia ni ngumu kwa jeshi kufanya lolote kwa sababu huwezi kujua f’lani amewekwa bond sehemu gani katika nchi au mji wake mkuu. Mfano, video ikisambaa mtandaoni wewe mwandishi umewekwa bond hapa Dar, nani atajua ni Mwanyamala?” kilihoji chanzo chetu.

KUMBUKUMBU  ZILIZOWAHI KUTIKISA

Amani lina kumbukumbu ya baadhi ya Watanzania waliowahi kuandikwa kwa madai ya kuwekwa bond ambao ni  Abdallah Mtoro ‘Dallas’ (alikombolewa), Sunday Dimonte (mume wa msanii Aunt Ezekiel, yupo gerezani) na Kanali Top (alikuwa mwanamuziki wa Bendi ya Akudo Impact).

Kanali Top aliwekwa bond nchini China, alipokombolewa akaamua kuifanya biashara hiyo mwenyewe, akadakwa na serikali na kunyongwa.

KAMANDA WA MADAWA YA KULEVYA

Juzi, Amani liliwasiliana na Kamanda wa Kikosi cha Kupambana na Kuzuia Madawa ya Kulevya Tanzania, ACP Mihayo Msikhela na kumuuliza kuhusu uwepo wa Wabongo wengi nje ya nchi wakiwa wamewekwa bond ambapo alisema:

“Ipo hivi, siwezi kusema sana kuhusu hilo, unajua wengi wanaifanya hiyo biashara. Sisi kama jeshi hatuna maelezo mengi bali nataka kuwaambia kuwa wote wanaofanya biashara hiyo haramu wakae wakijua hali imebadilika.

“Kwa sasa tuna mawasiliano na nchi nyingine mbalimbali duniani kuhakikisha kwamba, mtandao wa wauza unga unakufa haraka sana kwani biashara hiyo inapigwa vita duniani kote,” alisema kamanda huyo.

Leave a Comment