Bondia wa uzito wa juu Tyson Fury.

Tyson Fury (kulia) akiwa katika moja ya pambano.
BONDIA wa uzito wa juu Tyson Fury ameamua kukabidhi mikanda ya WBO na WBA ili kuelekeza nguvu katika matibabu ya afya yake ambayo haipo sawa kwa miezi kadhaa sasa.
Fury, 28, ameahirisha kupigana na Wladimir Klitschko mara mbili kutokana na kudai afya yake haipo sawa.
“Nafikiri ni sahihi na jambo zuri kwa mchezo wa ndondi ili kuwapa nafasi mabondia wengine waiwanie,” alisema Fury katika sehemu ya taarifa yake juzi.
