NIGERIA: Wanigeria wanaamini kuwa, mwanadada maarufu kwenye tasnia ya muziki kutoka nchini humo, Tiwa Savage ameuza roho yake na kujiunga na dini ya kishetani ili kufanikisha mambo yake ya kimuziki.
Ishu hiyo imesambaa kwenye mitandao ya kijamii nchini humo baada ya picha za ‘behind the scene’ za staa kuyo kuvuja zikionesha wakati aki-shoot kichupa cha wimbo wake mpya wa ‘Rewind’.
Picha hizo zinamuonesha Tiwa akiwa amekunja vidole vyake kuonesha ishara ambayo inadaiwa kuwa hutumiwa na dini ya kishetani jambo ambalo limezua mjadala nchini humo huku wadau na mashabiki wake wakimtuhumu kuwa baada ya kuhama lebo na kujiunga kwenye lebo ya Jay Z, Roc Nation basi mwanadada huyo huenda ‘ameuza roho’ yake na kujiunga na dini ya kishetani ili aweze kufanikisha mambo yake.
Mwanadada huyo ameachia video ya wimbo wake huo mpya wiki iliyopita ambapo picha hizo alizisambaza kwa ajili ya kufanyia promo.
Mashabiki wanaamini hizo ni ishara kuwa kwa sasa Tiwa anatumia nguvu za giza ili kufanikiwa malengo yake ya kimuziki na biashara.
Tiwa Savage – Rewind ( Official Music Video )