KATIBU wa Tume ya Utumishi wa Umma, Peleleja Masesa, amewaasa watumishi wa umma kuwa mfano wa kuigwa katika kazi na kuzingatia maadili na weledi wawapo kazini ili kujenga uadilifu kwa kutoa huduma inayostahili.
Viongozi hao wakisikiliza maswali ya wanahabari (hawapo pichani) yaliyokuwa yakiulizwa.
Hayo ameyasema leo alipokuwa akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam, ambapo mbali na kuwasisitiza pia alisema dhamira kubwa ya tume ni kuhakikisha watumishi wa umma wanatoa huduma bora kwa Watanzania na kutatua changamoto wanazokabiliana nazo.
Mkutano na wanahabari ukiendelea.
Na Denis Mtima/Gpl