The House of Favourite Newspapers

Angel Mary Kato: Nimerudi Kuwafunika Marapa wa Kike

1

 

MSHINDI wa nne wa michuano ya Bongo Star Search (BSS) ya mwaka 2015, Angel Mary Kato.
MSHINDI wa nne wa michuano ya Bongo Star Search (BSS) ya mwaka 2015, Angel Mary Kato, akiwa na mtangazaji wa Global Online Tv, Calvin Shayo

MSHINDI wa nne wa michuano ya Bongo Star Search (BSS) ya mwaka 2015, Angel Mary Kato, amerudi upya kwenye gemu ya Hip Hop na ameachia ‘audio’ ya kibao chake kipya kinachoitwa Cheza, huku video ya wimbo huo ikiwa bado ipo jikoni.
Angel ambaye kwa sasa yupo chini ya menejimenti ya ‘Simple The Boy Kiboko’ na ameachia ngoma mbili ambazo ni ‘No stress’ na hii mpya ya ‘Cheza’, amesema kuwa amejipanga vizuri ili kupambana na marapa wa kike nchini kama vile Chemical, Pink na Rosa Lee.
Angel alishika nafasi ya nne kwenye shindano la kumsaka msanii mwenye kipaji cha kuimba ambapo Kayumba Juma aliibuka mshindi wa kwanza akifuatiwa na Nassib Fonabo, Frida Aman, na mshindi wa tano alikuwa ni Kelvin Gerson.

NA ISRI MOHAMED/GPL

1 Comment
  1. […] miongoni mwa marapa wa kike waliokuwa wanachangamsha gemu ya Bongo Fleva kwa miaka ya nyuma basi huwezi kuacha kumtaja […]

Leave A Reply