The House of Favourite Newspapers

Mabinti wa Hip Hop Wasibaniwe, Watoboe!

KWA sasa huwezi kutaja maendeleo ya muziki wa kuchana kwa kinadada bila kumtaja mwanadada Onika Maraj ‘Nicki Minaj’.

Nicki ambaye unaweza kusema ndiye ‘top’ wa Muziki wa Hip Hop kwa sasa ulimwenguni amefanikiwa kwa kiasi kikubwa sana kuwafanya wadada nao waingie kwenye muziki huo.

Tammy katikati akiwa wadau wa muziki wakati wa maandalizi ya video ya wimbo wake.

Tangu alipoachia ngoma yake ya kwanza iliyomtoa ya Your Love inayopatika katika Albamu ya Barbie World Katika iliyotoka 2010, hakika Nicki ameweza kuwateka mamilioni ya wadada ambao nao wamejikuta wakivutika kwa kiasi kikubwa kurap.

Lakini ukiachana na Nicki, Kibongobongo Muziki wa Hip Hop kwa kinadada umeanza kuliteka soko mwanzoni mwa miaka ya 2000. Wapo wasanii wa kike waliokuwa wakipewa nafasi na kweli waliwika vilivyo.

 

Hadi sasa huwezi kuzungumzia muziki huo Bongo bila kutaja mchango waliotoa wakali wengine waliokuwa wakikimbizana kuachia ngoma kama vile, Fredinah Peyton a.k.a Rah P aliyewika na Ngoma ya Hayakuhusu, Zay B aliyewika na Gado, Sister P na Anakuja, Dataz na Mume wa Mtu.

Hata hivyo, wengine walikatishwa tamaa zaidi baada ya kuona kazi zao hazilipi kama vile ambavyo walikuwa wakitoa fedha studio kwa ajili ya kuzitengeneza.

Pengine sasa hivi ambao bado wanakomaa na gemu ya Hip Hop kwa akina dada ni Witness (Kibonge Mwepesi) aliyetokea Kundi la Wakilisha lililokuwa likiundwa na Shaa pamoja na Langa (marehemu) na Chiku aliyetokea Kundi la La Familia (limekufa) lililokuwa likiongozwa na Chid Benz likiwa na vichwa hatari kama Koba, Ditto, Kassim Mganga, Tunda Man na wengine kibao.

Kwa miaka ya hivi karibuni kimeibuka tena kizazi kingine kwa akina dada ambacho kinatisha kwenye Muziki wa Hip Hop Bongo, ukiwasiliza pengine ni wakali kuliko waliotangulia lakini ni dhahiri shahiri wanapata sapoti kiduchu kwenye spika za redio, runinga na magazeti.

 

Comments are closed.