Aussems Awaingia Sevilla na Mbinu Mpya

WAKATI kesho Alhamisi Simba wakiivaa Sevilla ya Hispania kwenye mechi ya kirafiki, kocha mkuu wa Simba, Patrick Aussems anaingia kwenye mechi hiyo akiwa na mbinu mpya ambayoameitambulisha ndani ya kikosi hicho kwa ajili ya kupunguza uchovu ‘fatiki’ kwa wachezaji wake.

 

Simba watacheza na Sevilla ambao wana historia ya kutwaa Kombe la Europa mara tatu mfululizo katika miaka ya karibuni katika mechi ya kirafiki ya kimataifa ambayo itapigwa katika Uwanja wa Taifa jijini Dar ikiwa ni mchezo maalum uliondaliwa na Kampuni ya Kubashiri Matokeo ya SportPesa.

 

Kabla ya kiuivaa Sevilla, Simba wikiendi iliyopita walicheza na Ndanda FC na jana Jumanne walicheza na Singida United lakini pia watacheza na Biashara United itakayopigwa Jumamosi hii kabla ya kumalizia na Mtibwa Sugar Mei 28. Kikosi hicho kitacheza mechi hizo zote katika kipindi cha siku 10 pekee.

Akizungumza na Championi Jumatano, Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amefunguka kwamba kocha Aussems kwa sasa anatumia njia ya kuwaingiza wachezaji wake kwenye maji baridi yenye barafu kwa ajili ya kuwafanya waondokane na uchovu pia kukwepa hali ya majeraha.

 

“Kwa sasa tuna mechi nyingi kwa kipindi kifupi hivyo kocha ameona aje na mbinu mbadala kwa ajili ya kukwepa majeruhi wa mara kwa mara kocha ameamua kila baada ya mechi kuna utaratibu mpya ambao anaufanya wa kuwaingiza wachezaji kwenye maji ambayo yana barafu.

 

“Hiyo ni mbinu kwa ajili ya kupooza miili na lakini pia inaondoa hali ya kupata majeraha kwa wachezaji kwa sababu katika kipindi hiki timu imekuwa ikicheza kila mara katika siku za karibuni hapa,” alisema Manara.

Said Ally, Dar es Salaam


Loading...

Toa comment