Azam FC Wakubali Kipigwe Bila Mashabiki
UONGOZI wa Azam FC umesema kuwa wao hawana shida ligi kuchezwa bila uwepo wa mashabiki, kwa kuwa jambo hilo limetokea kama dharura na hawana uwezo wa kupingana na maamuzi hayo.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Azam FC, Thabit Zakaria (Zaka za Kazi) ambaye ameeleza kuwa kilicho bora kwao kwa sasa ni kuona ligi inamalizika salama, wala hawatajali kucheza bila uwepo wa mashabiki kwa kuwa kila mmoja anajua uwepo wa Ugonjwa wa Covid-19 unaotokana na maambukizi ya Virusi vya Corona.
Akizungumza na Championi Ijumaa, Zaka alisema: “Kucheza ligi bila mashabiki hiyo ni dharura ni kama mko vitani hauchagui silaha iliyo karibu ndiyo unayotumia, kama tukisema kwenye vita hii silaha ni kucheza bila mashabiki wacha iwe hivyo.
“Mashabiki wakae nyumbani watapata taarifa kupitia vyombo vya habari lakini mimi ningependa ichezwe iwe kwa kituo rasmi siyo ichezwe nchi nzima kama ilivyokuwa timu mnasafi ri mnakwenda huku nadhani hiyo itakuwa hatari zaidi.


