The House of Favourite Newspapers

BASATA WAKANUSHA KUWASAMEHE DIAMOND NA RAYVANNY

 

Diamond Platnumz na Rayvanny.

Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA)  limekanusha kuwafungulia wasanii Diamond Platnumz na Rayvanny wanaotumikia adhabu ya kutojihusisha na muziki kwa muda usiojulikana baada ya kufanya makosa mbalimbali ndani ya kipindi cha miezi miwili.

 

Taarifa hiyo imekuja baada ya msanii Diamond kutangaza kwenye mkutano wa waandishi wa habari jana kuwa wameruhusiwa kufanya tamasha la muziki, Wasafi Festival’  nchini Kenya.

 

Siku ya jana Desemba 21, wasanii hao kupitia mtandao wa Instagram waliomba radhi kwa mamlaka mbalimbali nchini na jioni walionekana wakifanya mkutano na wanahabari Nairobi nchini Kenya kutangaza maonyesho yao yanayoendelea, lakini alifajiri taarifa ya Basata ilisema kuwa hawajatoa ruhusa kwa wasanii hao.

 

“Ikumbukwe kuwa Desemba 18 tuliwafungia kutojihusisha na sanaa kwa kipindi kisichojulikana kwa kuimba kwa makusudi wimbo Mwanza tulioufungia kwa sababu za kimaadili,

“Baraza linasisitiza kuwa halijawafungulia wasanii hao, pia linawaonya kuacha kutoa taarifa za uongo kabla halijawachukulia hatua kali zaidi,” imeeleza barua hiyo.

 

#ISIKUPITE : SHERIA 10 za KANYE WEST kwa Mkewe KIM KADARSHIAN

 

 

Comments are closed.