The House of Favourite Newspapers

BREAKING: Mtolea Akichukua Fomu ya Ubunge Temeke – VIDEO

Aliyekuwa Mbunge wa Temeke kwa tiketi ya Chama cha Wananchi CUF, Abdallah Mtolea, amechukua tena fomu ya kugombea Ubunge katika chama hicho ikiwa ni wiki chache zimepita tangu atangaze kujiuzulu nafasi yake ya Ubunge akiwa ndani ya ukumbi wa Bunge.

 

Mtolea alitangaza kujiuzulu nafasi yake hiyo na kisha kukihama chama chake cha CUF na kujiunga na CCM, Ambapo Katibu mkuu wa CCM, Dkt Bashiru Ally, amempa nafasi ya kugombea Ubunge kwenye jimbo hilo kwa mara nyingine.

 

Akizungumza baada ya kupokea fomu ambazo anatakiwa kuzijaza na kisha kuzirejesha katika ofisi za zinazosimamia uchaguzi kesho Desemba 20, Mtolea amewaomba wananchi wa Temeke kumpokea kwa mara nyingine tena.

 

BREAKING: Mtolea Achukua Fomu ya Ubunge Temeke!

Comments are closed.