The House of Favourite Newspapers
gunners X

Mbunge Jenista Mhagama, Afariki Dunia Leo, Dodoma

0

Aliyekuwa Mbunge wa Peramiho, Jenista Joakim Mhagama.

Mbunge wa Peramiho, Jenista Joakim Mhagama, amefariki dunia leo 11 Desemba 2025 jijini Dodoma. Taarifa hiyo imetolewa na Spika wa Bunge la Tanzania, Mussa Azzan Zungu, ambaye amesema kuwa Bunge limepokea msiba huo kwa masikitiko makubwa.

Spika Zungu ametuma salamu za pole kwa Wabunge, familia, ndugu, jamaa, pamoja na wananchi wa Jimbo la Peramiho. Aidha, amewaomba Mungu awape nguvu na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu.

Taarifa kutoka Ofisi ya Bunge zinaonyesha kuwa mpango wa mazishi ya Jenista Mhagama utatolewa kwa kushirikiana na familia yake, huku mashabiki na wananchi wakitarajia kuwa na nafasi ya kumkumbuka na kumzika kwa heshima zinazostahili kiongozi wa taifa.

Leave A Reply