The House of Favourite Newspapers

Breaking: Wabunge Waitwa Bungeni Dodoma

0

Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Nenelwa Mwihambi leo Ijumaa, Januari 7, 2022 amesema baada ya Job Ndugai kujiuzulu nafasi ya Uspika kwa sasa taratibu za uchaguzi wa kujaza nafasi hiyo zinaendelea na kwamba kwa mujibu wa sheria kiti cha Spika kinapokuwa wazi hakuna shughuli yoyote itakayotekelezwa katika Bunge isipokuwa Uchaguzi wa Spika.

 

Katika taarifa yake, Mwihambi amesema Kamati zilizokuwa zikutane kianzia Januari 10, 2022 na Januari 17, 2022 hazitokutana kwa wakati huo na badala yake zitakutana wakati wa Mkutano wa Sita wa Bunge Februari 1-11, 2022 kwa utaratibu wa tarehe zitakazotangazwa na hivyo Wabunge wameombwa kufika Dodoma Januari 31, 2022.

 

Leave A Reply