The House of Favourite Newspapers

CAF Yawafungulia Mtibwa Michuano ya Kimataifa

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limesema limepokea barua kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu Africa CAF inayoelezea kuwa Klabu ya Mtibwa Sugar imemaliza adhabu yake ya kufungiwa lakini ikitakiwa kuthibitisha kwa maandishi malipo ya faini ya dola za Marekani 1500 na fidia kwa klabu ya Santos ya Africa Kusini ili kuiwezesha kushiriki mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa TFF, Kidao Wilfred amesema Mtibwa watapaswa pia kulipia gharama za safari ya klabu ya Santos ya Afrika Kusini kabla ya Julai 20 2018.
Ikumbukwe Mtibwa Sugar ilifungiwa na CAF kwa muda wa miaka mitatu kushiriki mashindano yake kutokana na kushindwa kupeleka timu Afrika Kusini kwa ajili ya mchezo dhidi ya Santos.
Kwa mujibu wa Kaimu Katibu Mkuu wa TFF, Wilfred Kidao, amesema Mtibwa wanapaswa kuwajibika na gharama hizo za Santos pamoja na faini hiyo ili waweze kupata tiketi hiyo ya ushiriki wa mashindano hayo.
Mtibwa Sugar ilipata nafasi ya kuikwakilisha Tanzania kwenye mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kuibuka bingwa wa kombe la FA dhidi ya Singida United kwa ushindi wa mabao 3-2 kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.

Comments are closed.