The House of Favourite Newspapers

Chirwa, Ngoma pasua kichwa Azam

KOCHA Msaidizi wa Azam FC, Idd Cheche ameweka wazi kuwa tatizo kubwa ambalo linaipasua timu hiyo ni washambuliaji wake kutotumia vyema nafasi wanazopata.

 

Safu ya ushambuliaji ya Azam FC inaongozwa na Obrey Chirwa, Donald Ngoma pamoja na Idd Seleman ‘Naldo’.

 

Azam FC ina kibarua cha kumenyana na Triangle United ya Zimbabwe, Septemba 15, kwenye Uwanja wa Chamazi ambao ni wa Hatua ya Kwanza ya Kombe la Shirikisho Afrika.

 

Akizungumza na Championi Jumamosi, Kocha Msaidizi wa Azam FC, Idd Cheche alisema kuwa tatizo kubwa ambalo ni pasua kichwa ndani ya Azam FC ni umaliziaji wa nafasi kwa wachezaji.

 

“Tumegundua tatizo pale lilipojifi cha jambo ambalo limetufanya tutumie muda mwingi kulifanyia kazi kwa kurudia mara kwa mara, safu ya ushambuliaji imeanza kuleta matumaini mapya na tuna Imani kabla ya mchezo wetu wa kimataifa tutakuwa sawa.

 

“Tumeanza kuinoasafu ya ushambuliaji kwa kutumia michezo ya kirafi ki ambapo kwenye michezo miwili tumefunga jumla ya mabao sita nasi tukifungwa bao moja hapo kuna kitu kimeongezeka,” alisema Cheche.

Lunyamadzo,, Dar es Salaam

Comments are closed.