CUF Ya Maalim Seif Yamwomba Lipumba Asiwavuruge Wanachama

 

Mwenyekiti wa Tawi la Mwinyimkuu Kigogo, Rashid Abdullah akizungumza na wanahabari.

VIONGOZI wa Matawi ya Hamasa Mkoa wa Dar es Salaam wanaomuunga mkono Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF) Maalim Seif Sharif Hamad leo wamemwomba Prof. Ibrahim Lipumba kuacha mara moja kuwavuruga wanachama wa chama hicho kwa madai ya kuwa wajumbe wa chama hicho kupitia mkutano wake wa Agosti 8, mwaka huu waliridhia kujiuzulu kwake kwa asilimia 74 na hivyo si mwenyekiti tena.

Walisema kuwa Lipumba na baadhi ya wafuasi wake wamekuwa wakivamia ofisi kuu ya chama hicho iliyopo Buguruni jijini Dar es Salaam kwa lengo la kukihujumu na kukisambaratisha kwa kuwaaminisha baadhi ya wanachama wamtambue kuwa yeye ndiye mwenyekiti wa taifa wa chama hicho.

Mkutano na wanahabari ukiendelea.

Akisisitiza jambo hilo, leo jijini Dar es Salaam,  Mwenyekiti wa tawi la Mwinyimkuu-Kigogo, Rashid Abdullah, alipokutana na wanahabari alisema wamekuwa kimya wakiangalia sinema nzima ya Lipumba na kila alichoita genge lake ambapo  wamegundua  tayari anatumiwa na CCM kukihujumu  chama ili kisiweze kushinda uchaguzi wa serikali za mitaa, vijijini  na vitongojini  mwaka 2019.

Mjumbe wa Tawi la Kosovo Kassim Chongamawano akifafanua jambo.

“Lipumba na genge lake anatumiwa na CCM kuzima harakati za chama zinazofanywa na Katibu Mkuu, Maalim Seif Sharif Hamad, katika uchaguzi mkuu wa 2015 na kupunguza nguvu za pamoja za vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) kwa lengo la kuisaidia CCM”.

Alimtaka Lipumba aache mara moja kuendelea kuvuruga chama kwani tayari maamuzi ya chama kupitia kikao chake halali cha Baraza kuu kilichofanyika Zanzibar kilimfukuza uanachama na hapaswi kuendelea kukiharibu chama.


Loading...

Toa comment