The House of Favourite Newspapers

Exclusive! Wema Aibuka na Kipigo cha Mondi

0

KWA walioimisi ile kapo ya kihistoria Bongo ya mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na mrembo mwenye nyota zake mjini, Wema Isaac Sepetu wasipate taabu sana, imekuja kivingine, IJUMAA WIKIENDA linakushushia habari mpya inayowahusu.

NI WEMA MWENYEWE…

Habari hiyo si ya kutoka hewani au kwa watu wa karibu, bali ameiibua mwenyewe mrembo huyo ambapo ameeleza kinagaubaga jinsi ambavyo anamhusudu Diamond au Mondi hasa anapokumbuka matukio ‘waliyoshea’ pamoja wakati penzi lao lilipokuwa ‘fire’.

NI EXCLUSIVE

Akizingumza na Gazeti la IJUMAA WIKIENDA kwenye mahojiano maalum (exclusive), mbali na kuzungumzia kuhusu mpenzi wake huyo wa zamani (eksi) na kipigo chake, pia Wema amezungumzia mambo mengine mbalimbali yanayomhusu.

TUJIUNGE NAYE…

IJUMAA WIKIENDA: Mambo vipi Wema, habari za siku nyingi?

WEMA: Salama kabisa, nipe habari maana najua lazima una kitu, si kwa kunisaka huko.

IJUMAA WIKIENDA: Hakuna ila nimeona uko kimya, nikasema nikutafute kujua kulikoni?

WEMA: Mimi nipo, lakini nipo bize kidogo na kazi, narekodi sasa hivi labda nikimaliza nitakuwa nimetulia.

IJUMAA WIKIENDA: Nilijua labda umeachana na mambo ya sanaa kwa sasa kumbe bado unakomaa?

WEMA: Hapana, kwa nini sasa niache kitu ninachokipenda? Yaani nitakomaa mpaka hilo soko la muvi liombe poo.

IJUMAA WIKIENDA: Siku za hizi umebadilika sana, siyo mtu wa kutokatoka kwenda kwenye viwanja vya starehe kama ilivyokuwa huko nyuma, nini shida?

WEMA: Yaani huwezi kuamini, kila mwaka unavyoongeza miaka yako ndivyo unavyojitengeneza kuwa tofauti kila siku. Kuna vitu tu huwezi kuvifanya kabisa, unaangalia vitu vingine vinavyoendana na wewe ulivyo, lakini kwenye mitoko ya muhimu sana natoka.

IJUMAA WIKIENDA: Kipindi hiki umekuwa mtu ambaye umeyaficha sana uhusiano wako wa kimapenzi tofauti na ilivyokuwa huko nyuma, ni kwa nini labda?

WEMA: Niameamua kufanya hivyo kwa sababu nimetaka kubadilisha mfumo wa maisha yangu kabisa hivyo kuna mambo yangu mengine nayafanya siri sana.

KIPIGO SASA…

IJUMAA WIKIENDA: Tukirudi nyuma, ni kitu gani unakikumbuka kutoka kwa Diamond wakati wa mapenzi yenu?

WEMA: Kipigo chake tu.

IJUMAA WIKIENDA: Kwa nini unakumbuka kipigo chake, kilikuwaje?

WEMA: Aisee kilikuwa hatari, lakini nilikuwa napenda kupigwa naye kwa kweli yaani sijui nisemeje, kwa sababu alikuwa akinipiga ananibembeleza sana, basi nainjoi. Kiukweli nakimisi kipigo kama kile na kubembelezwa.

IJUMAA WIKIENDA: Kipigo gani unakikumbuka kutoka kwake?

WEMA: Kuna siku Nasibu (Mondi) alionaga meseji imeingia kwangu akawa ana wasiwasi nayo, akanipiga kibao kikali kwenye shavu, halafu ndugu zangu wakajua na hata ninyi (Magazeti Pendwa) mlitoa kwenye gazeti, lakini niliwaambia mimi napenda kupigwa naye hivyo waniache.

IJUMAA WIKIENDA: Na ni kweli ulikuwa unapenda kupigwa naye au uliwajibu tu ndugu zako?

WEMA: Hapana, ni kweli kabisa hasa mimi nikipenda ndivyo nilivyo.

IJUMAA WIKIENDA: Vipi yeye Diamond, anajua hilo?

WEMA: (kicheko) anajua sana, kwa nini asijue.

IJUMAA WIKIENDA: Haya Wema, nashukuru sana kwa ushirikiano wako.

WEMA: Asante sana karibu tena na tena.

TUJIKUMBUSHE

Wema na Mondi ilikuwa ni kapo iliyotokea kupendwa mno Bongo, lakini baadaye walimwagana na kila mtu aliendelea na maisha yake, japokuwa walikuwa na tabia ya kuachana na kurudiana.

Lakini tangu walipoachana mara ya mwisho, imepita miaka mingi sasa ambapo Mondi aliendeleza safari yake na wanawake wengine hadi kufanikiwa kupata watoto wanne kwa mama tofauti.

LOLOTE LAWEZA KUTOKEA

Kutokana na Wema kukiri mara kwa mara kuwa anamkubali sana Mondi na kwa vile staa huyo Jeje hana mtu kwa sasa, wakiamua wanaweza kufanya jambo na mashabiki wakarejea kwenye kapo ya mioyo yao!

STORI: IMELDA MTEMA, DAR

Leave A Reply