FAIZA AFURAHIA SUGU KUPATA MTOTO

TOFAUTI na matarajio ya wambeya wa Instagram, kwamba mzazi mwenziye Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’, Faiza Ally atakuwa na kinyongo na mwanamke wa sasa wa Sugu, mrembo huyo amewakata maini mashabiki wa mtandao huo kwa kuonesha hana kinyongo.

 

Juzikati shabiki mmoja anayejiita Nancy_naaa alianzisha mjadala Instagram kwa kumuuliza Faiza kama ana habari za mke mwenziye kujifungua mtoto wa kiume ndipo Faiza alipomwambia aache umbeya maana taarifa anazo.

 

“Hii ni kuwajulisha wewe na wambeya wenzio kwamba najua na nimefurahi Sasha amepata kaka alhamdulilhah mama na mtoto wanaendelea vyema,” aliandika Faiza.


Loading...

Toa comment