HEMED HANA TIME NA WADADA WA BONGO MUVI

MSANII wa filamu za Kibongo, Hemed Suleiman ‘PHD’ amefunguka kuwa hajawahi kumshobokea staa yeyote wa kike ndani ya Bongo Muvi na hatafanya hivyo.  Staa huyo, alisema wanawake wengi wanafikiri kuwa anaringa na kujisikia lakini ukweli ni kwamba hajaona wa kutoka naye Bongo Muvi ndiyo maana anawapigia kimya.

“Hili nalisema kila wakati, ningekuwa na mizuka na mastaa kwa kweli ningetembea nao wengi, lakini mimi sitaki kwa sababu bado sijaona wa kutoka naye… cha msingi nafurahi tayari nina watoto wangu, hilo nashukuru Mungu,” alisema Hemed.


Loading...

Toa comment