JKT: Simba Ilitolewa Kimakosa Ligi ya Mabingwa

KOCHA Mkuu wa JKT Tanzania, Mohamed Abdallah ‘Bares’ amesema kuwa kikosi cha Simba kimetolewa kwa makosa ya wachezaji kushindwa kutumia nafasi walizozipata kwani uwezo wao ni mkubwa.

 

JKT Tanzania iliambulia kichapo cha mabao 3-1 mbele ya Simba kwenye mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu Bara uliochezwa uwanja wa Uhuru, juzi. Simba iliondolewa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya UD Songo ya Msumbiji kufuatia kwa faida ya bao la ugenini.

 

Akizungumza na Championi Jumamosi, Bares alisema kuwa aliutazama mchezo wa Simba dhidi ya UD do Songo na kuona namna walivyocheza kwa kushindwa kutumia makosa ya wapinzani jambo ambalo limeiponza pia timu yake.

 

“Nimeponzwa kwa kushindwa kutumia nafasi ambazo wachezaji wangu walizipata kwenye mchezo kama ambavyo ilitokea kwa Simba kushindwa kupenya mbele ya UD Do Songo huu ni mpira na haya ni matokeo.

 

“Kwa sasa maisha lazima yaendelee makosa ambayo tumeyafanya tunakwenda kuyarekebisha na kuyafanyia kazi kwa ajili ya wakati ujao ligi bado inaendelea,” alisema Bares.

Lunyamadzo Mlyuka Dar es Salaam


Loading...

Toa comment