The House of Favourite Newspapers

Kiungo wa Rivers United Morice Chukwu Aandaliwa Mkataba Yanga

0
Morice Chukwu

UONGOZI wa Yanga tayari umepewa jina la kiungo wa kati wa timu ya Rivers United Morice Chukwu kutoka kwenye benchi  la ufundi la timu hiyo kwaajili ya usajili wa dirisha kubwa mwishoni mwa msimu huu

Chukwu, 20, katika mchezo uliopita wa Yanga dhidi ya Rivers United alionyesha kiwango kizuri ambacho kilipelekea kocha Nabi kuongea naye mara baada ya mpira kumalizika.

Kocha Nabi alionekana kuzungumza na mchezaji huyo kwa dakika mbili akiwa na Meneja wa Yanga, Walter Harryson baada ya mpira kumalizka na kuwashtua watu wengi wakiamini kuna jambo litatokea.

Chanzo chetu cha ndani kutoka Yanga kimeliambia Championi Jumatano juu ya suala la mchezaji huyo tayari kupelekwa kwa uongozi wa Yanga kwa ajili ya usajili wa dirisha kubwa na kufuatiliwa mwenendo wake kwa ujumla ili ujiridhishe juu ya uwezo wake.

“Tayari uongozi umepelekewa jina la mchezaji huyo kutokana na uwezo mkubwa ambao ameuonyesha mchezaji huyo katika michezo ya Kombe la Shirikisho iliyofanyika msimu huu, benchi la ufundi limependekeza kuendelea kufanyiwa maangalizi ya maendeleo yake kwaajili kujiridhisha zaidi kabla ya usajili.

“Kiufupi benchi la ufundi wamevutiwa na uwezo wa mchezaji huyo na ndio maana utaona baada ya mchezo kumalizika walikwenda kuzungumza naye na hii sio mara ya kwanza kutokea, imewahi kutokea kwa baadhi ya wachezaji ambao wamekuja kwa kuongea na benchi la ufundi ambalo uongozi wa Yanga unaawaamini kwa asilimia kubwa.

“Kiufupi tunatarajia mambo mazuri katika dirisha kubwa kwa kuwa kuna wachezaji tayari wameshakabidhiwa kwa benchi la ufundi,” alisema kiongozi huyo.

Na Marco Mzumbe

YANGA vs MARUMO GALLANTS, GEORGE JOB AWAPA NAFASI YANGA KUTINGA FAINALI CAF…| UCHAMBUZI

Leave A Reply