The House of Favourite Newspapers

Kwasi Aikomalia Simba

BEKI wa kushoto wa Simba, raia wa Ghana, Asante Kwasi, ameonyesha hali ya kuigomea klabu hiyo akisisitiza hayupo tayari kuondoka kizembe Msimbazi, hata kama watahitaji kumtoa kwa mkopo.

 

Kwasi alijiunga na Simba kwenye dirisha dogo la usajili msimu uliopita akitokea Lipuli FC ya Iringa, kwa mkataba wa miaka miwili ambapo mkataba wake unatarajiwa kumalizika Desemba, mwaka huu, huku mchango wake ndani ya klabu hiyo ukiendelea kuwa mdogo zaidi.

 

Akizungumza na Championi Ijumaa, Kwasi alisema, pamoja na mkataba wake wa kuitumikia Simba kubakiza miezi mitano tu, hatakubali kuiacha kizembe hata kama viongozi wake watataka kumtoa kwa mkopo.

 

“Napenda sana kuendelea kuitumikia Simba kwa msimu ujao, pamoja na kuwa na muda mfupi wa kucheza kwa sasa, siko tayari kuiacha Simba, ila nitajitahidi kupambana kadiri ninapopewa nafasi za kucheza na kocha ili nionyeshe mchango hasa kwa msimu ujao kwani msimu huu umekuwa mgumu kwangu baada ya kukabiliwa na majeraha ya mara kwa mara.

HAJI MANARA Atoa Taarifa SIMBA Watakavyopokea Kombe kwa Msafara

Comments are closed.