Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Oeo amezindua rasmi Jeshi USU litakalokuwa na majukumu ya kulinda wanayama Pori na rasilimali za misitu hapa nchini ikiwa ni hatua ya serikali kuimalisha ulinzi katika rasilimali za taifa.
Jeshi hilo limeundwa kwa makusudi na serikali katika kupambana na ujangili hasa kwa wanyama wanaojulikana kama big 5 ambao ni FARU, SIMBA,TEMBO, NYATI na CHUI.
Akihutubia katika uzinduzi huo uliofanyika katika eneo la Fort Ikoma wilayani Serengeti Mkoani Mara, Makamu wa Rais amewataka askari hao wakafanye kazi kwa kuzingatia sharia na weledi ili kulinda rasilimali za nchi
Kwa upande wake Mjumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira Nape Nnauye amewataka askari wa Jeshi hilo kuzingatia haki za binadamu wakati wa kufanya oparesheni zao maeneo mbalimbali.
Kuzinduliwa kwa Jeshi Usu la wanyamapori ni utekelezaji wa sharia namba 5 ya wanyamapori ya mwaka 2009 ambayo inaitaka wizara ya Maliasili na Utalii kuwa na vyombo vya Ulinzi wa rasilimali za taifa.
Comments are closed.