Leo Julai 25, 2017, Rais John Magufuli anaendelea na ziara yake na leo yuko wilayani Itigi mkoani Singida kufungua Barabara ya Manyoni – Itigi – Chaya yenye kilomita 89.3.
Hadi sasa viongozi kadhaa wa kiserikali wameshazungumza akiwemo Mwigulu Nchemba na miongoni mwa mambo aliyogusia, ametaka wanaoacha mawe barabarani baada ya kutengeneza magari yao wakamatwe.
Fuatana nami kutoka Itigi, Singida kujua kitachojiri
#JPMSingida: Hakuna mtumishi wa afya atakayethubutu kuiba dawa tukamuacha. Tutamnyang’anya leseni na kummaliza kabisa –@HKigwangalla pic.twitter.com/AWO02aObCl
— Global Publishers (@GlobalHabari) July 25, 2017
#JPMSingida:Viongozi karibu wote na watumishi 3000 wameshahamia Makao Makuu Dodoma, mimi na makamu wangu tutahamia hivi karibuni.@MagufuliJP pic.twitter.com/PYD6TOHPmM
— Global Publishers (@GlobalHabari) July 25, 2017
#JPMSINGIDA: Wanaopiga kelele kuhusu hili la madini, wamepewa rushwa, ukiona tochi imewaka ujue kuna betri ndani yake. –@MagufuliJP pic.twitter.com/GaWzQ1MbUj
— Global Publishers (@GlobalHabari) July 25, 2017
#JPMSingida: Ni bora tununue mitambo tuchimbe wenyewe madini yetu tutatajirika, kuliko wizi uliokuwa unafanywa na wawekezaji. –@MagufuliJP
— Global Publishers (@GlobalHabari) July 25, 2017
#JPMSingida: Tumenunua ndege nchini Marekani, inaweza kubeba watu 262, inaweza kutoka Marekani hadi Tanzania bila kutua, tutaileta mwakani. pic.twitter.com/54oliBY1Hh
— Global Publishers (@GlobalHabari) July 25, 2017
#JPMSingida: Tumeamua siku hii ya mashujaa isiwe ya masherehesherehe ili mashujaa wenzao walio hai wafanye kazi na kuwaombea – @MagufuliJP
— Global Publishers (@GlobalHabari) July 25, 2017
#JPMSingida: Kuna Watanzania hapa ambao wamejenga mahoteli nje ya Tanzania, lakini nyumba za wazazi wao zimechakaa mno – Rais @MagufuliJP.
— Global Publishers (@GlobalHabari) July 25, 2017
#JPMSIngida: Serikalini huko walikuwepo watu wapigaji dili hadi wamesahau kabisa kama kuna Mungu- Rais @MagufuliJP.
— Global Publishers (@GlobalHabari) July 25, 2017
#JPMSingida:Wengine mmewachagua lakini wanaongelea ya mambo D’Salaam tu kosea kuoa unaweza kutoa talaka lakini usikosee kuchagua-@MagufuliJP
— Global Publishers (@GlobalHabari) July 25, 2017
#JPMSIngida: Tumetatua changamoto ya madawati nchi nzima, sasa hivi hata watoto wa @TunduLissu wanakalia madawati- Rais @MagufuliJP pic.twitter.com/s0XQNJinVu
— Global Publishers (@GlobalHabari) July 25, 2017
#JPMSingida: Niliporudishwa Wizara ya Ujenzi nilimfukuza Chief Executive Officer ndani ya siku 3 kwa matumizi mabaya ya fedha- @MagufuliJP
— Global Publishers (@GlobalHabari) July 25, 2017
#JPMSingida: Watanzania nataka mjue kuwa wizara ambayo bado sijatoka ni Wizara ya Ujenzi, naitazama kwa jicho la mbali- Rais @MagufuliJP.
— Global Publishers (@GlobalHabari) July 25, 2017
#JPMSingida: Msiache bonde hata moja, lima hata nyanya, matikiti, ufuta au chochote, kitakusaidia baadaye. @MagufuliJP
— Global Publishers (@GlobalHabari) July 25, 2017
#JPMSingida: Kuna wengine kazi yao ilikuwa kusimama na karatasi barabarani kudai ushuru, sasa hivi akikuuliza ushuru mwambie ushuru na wewe.
— Global Publishers (@GlobalHabari) July 25, 2017
#JPMSingida: Sitatoa chakula cha msaada, RC au DC ambaye eneo lake litakuwa na njaa nitamtoa kwa kuwa amejidhihirisha hawezi kuhimiza kazi.
— Global Publishers (@GlobalHabari) July 25, 2017
Wananchi waliojenga kwenye hifadhi ya reli waanze kujiandaa kisaikolojia, wanaweza tu kuanza kubomoa taratibu nyumba zao- @MagufuliJP
— Global Publishers (@GlobalHabari) July 25, 2017
@MagufuliJP: Serikali ilikuwa ikiingia kwenye ubia makampuni watapeli, viwanda na wameviua, lazima haya yote niyatapike wajijue #JPMSingida:
— Global Publishers (@GlobalHabari) July 25, 2017
JPM SINGIDA: Rais Magufuli amezindua rasmi barabara ya Manyoni–Itigi-Chaya yenye urefu wa kilometa 89.3 mkoani Singida, ili ianze kutumika. pic.twitter.com/GMxp95eqB0
— Global Publishers (@GlobalHabari) July 25, 2017