The House of Favourite Newspapers

MAHAKAMA YAKUBALI ZUIO DHIDI YA WADHAMINI CUF-LIPUMBA

Baadhi ya wafuasi wa CUF pande za Lipumba na Maalim Seif wakiwa Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam leo.

 

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam imekubali maombi ya zuio la muda dhidi  Bodi ya Wadhamini ya CUF inayomuunga mkono Mwenyekiti anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Profesa Ibrahim Lipumba, katika shauri lililowasilishwa mahakamani hapo na Mbunge wa Malindi (CUF), Ally Salehe.

 

Jaji wa Mahakama Kuu, Jaji Wilfred Ndyansobera ameipiga mafuruku bodi hiyo kufanya shughuli zozote zinazohusu chama cha CUF hadi shauri la msingi namba 13/2017 litakapomalizika.

Ndyansobera  ametoa uamuzi huo mdogo baada ya kupitia hoja za mawakili wa pande zote mbili na kujiridha kwamba maombi ya muombaji yalikuwa na nguvu kisheria na kukidhi masharti yaliyowekwa kwenye kesi.

 

Awali Jaji Ndyansobera aliyatupilia mbali maombi ya mawakili upande wa walalamikaji wakiongozwa na  wakili Gabriel Malata ya kumtaka jaji asisome maamuzi hayo kwa madai kuwa wanakusudia kukata rufaa katika Mahakama ya Rufaa juu ya maamuzi ya Jaji Ndyansobera ya  kukataa kujitoa katika kusikiliza mashauri ya CUF, ambapo alisema  hakuna hoja za kisheria zinazozuia mahakama kuacha kuendelea na shughuli zilizopangwa.

 

NA DENIS MTIMA/GPL

Comments are closed.