Mama Kanumba: Huyu Ndiye Mrithi wa Kanumba, Naamini Atanifuta Machozi!

  fredy-mrithi-wa-kanumba-4Na Mayasa Mariwata, Risasi Mchanganyiko, Toleo la Jumatano, Jan. 11, 2017

DAR ES SALAAM: Wakati ikiwa inakaribia miaka mitano tangu  Aprili 7, 2012, ambapo aliyekuwa nguli wa filamu Bongo, Steven Kanumba, alipoaga dunia, mama yake mzazi Bi. Flora Mtegoa ametembelea kaburini kwa marehemu mwanaye siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwake akiwa ameambatana na kijana aliyemuanika kuwa ndiye mrithi wa muigizaji huyo nambari one nchini.

fredy-mrithi-wa-kanumba-1

Mama Kanumba akiweka kadi ya kumbukumbu kwenye kaburi la nmwanaye.

Katika makaburi ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam Jumapili iliyopita, mama huyo alisema siku ya kwanza kuonana na kijana huyo aliyemtaja kwa jina la Fredy Swai, alipatwa na mshtuko mkubwa kwa sababu alimuona anafanana mno na mwanaye, tofauti na watu wengine ambao mara kadhaa wamekuwa wakifananishwa na mkali huyo wa filamu Tanzania.

kanumbaaa222

Kanumba (kulia enzi za uhai wake) na mrithi wake Fredy.

fredy-mrithi-wa-kanumba-10Mama Kanumba na mrithi wa mwanaye wakiwa kwenye kaburi la marehemu Kanumba.

Fredy ambaye ni msanii wa Tamthilia ya Dhamira inayorushwa katika kituo cha televisheni cha ITV, ameelezewa na mama huyo kuwa anafanana mno na mwanaye na kwamba anaamini atamfuta machozi siku zote za maisha yake.

fredy-mrithi-wa-kanumba-7Mrithi wa Kanumba, Fredy akiwa pembezoni mwa kaburi la nguli huyo wa filamu Bongo.

Akimzungumzia kijana huyo, alisema alipigiwa simu na kuambiwa juu ya mfanano huo na siku alivyokwenda nyumbani kwake Kimara Temboni, aliamini faraja yake iliyopotea imerejea upya.

steven-kanumba

StevenKanumba enzi za uhai wake.

“Nimeona ninunue kadi niweke kwenye kaburi la mwanangu kumuenzi kwa maombi, sikutaka kusumbua watu ndiyo maana unaona nimeambatana na vijana wangu wawili tu, huyu Fredy tangu nimfahamu najihisi kama namuona mwanangu, nimekubali kuwa wanafanana sana hao wengine sijawapitisha.fredy-mrithi-wa-kanumba-6

fredy-mrithi-wa-kanumba-2Kadi aliyoandika mama Kanumba na kuiweka kwenye kaburi la mwanaye.

“Kila ninapofika hapa kaburini huwa machozi hayakauki, lakini leo ni tofauti na siku zote, chozi langu halijadondoka, sababu nimempata mrithi wake, mtu ambaye ananifanya nisilie tena, nampenda kama Kanumba, naamini atafuata nyayo zake kwenye sanaa,” alisema mama huyo.fredy-mrithi-wa-kanumba-5

Wakiwa makaburini hapo, mambo matatu muhimu yalifanyika, ikiwa ni kusafisha kaburi hilo, kufanya maombi ya kumtakia mema huko aliko, sambamba na kuweka shada la maua na kadi kwa kumuenzi.

fredy-mrithi-wa-kanumba-3Kwa upande wake, Fredy alisema, amekuwa akipata usumbufu mkubwa kwa kufananishwa na Kanumba na mara nyingi amekuwa akiitwa jina la Steve, ndipo watu wakamshauri amtafute mama huyo kwa kuamini anaweza kufarijika akimuona.

fredy-mrithi-wa-kanumba-11“Tangu utotoni, watu walikuwa wanawaambia wazazi wangu wanipeleke kwa Kanumba nikacheze kama mdogo wake, nikawa naogopa kuonana naye kutokana na ustaa aliokuwa nao marehemu,” alisema chipukizi huyo.fredy-mrithi-wa-kanumba-12

Fredy akiwa kwenye kaburi la Kanumba.

Mama Kanumba: Huyu Ndiye Mrithi wa Kanumba, Naamini Atanifuta Machozi!

 

Stori zinazo husiana na ulizosoma

Toa comment