The House of Favourite Newspapers

Manchester United Kufyeka Mastaa 14

KOCHA wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer ametoa muda wa miezi 12 kwa klabu hiyo kuwaondoa wachezaji wote wanaobo ronga katika timu hiyo.

 

Solsksjaer ameoro dhesha wachezaji 14 kuwa hawafai kuchezea timu hiyo na wanapaswa kuondoka. Manchester United tayari imeanza kuondoa baadhi ya mastaa mbalimbali ikiwa sehemu ya mpango wa kusuka upya kikosi hicho.

Mastaa ambao tayari wamefungasha virago ni pamoja na Antonio Valencia na Ander Herrera wakati Marcos Rojo na Matteo Darmian wanatazamiwa kuondoka wakati wowote.

 

Pia Solskjaer inasemekana anataka mastraika Romelu Lukaku na Alexis Sanchez wauzwe pia. Lukaku anatakiwa na Inter Milan, ambayo inatazamiwa kumchukua Antonio Conte kama kocha wake mpya.

 

Sanchez naye amegeuka mzigo kwani analipwa mshahara mkubwa wa pauni 400,000 (Sh. bilioni 1.2) lakini ameshindwa kuonyesha makali yake uwanjani.

Comments are closed.