The House of Favourite Newspapers

Mashabiki Walonga na Championi, Waifungukia Yanga na Simba

1

 

NAWAPONGEZA sana Championi kwa juhudi zenu za kutuhabarisha ila ushauri wangu kurasa zote naomba ziwe za rangi siyo kuweka kwenye baadhi ya kurasa.

Nelly Kazimili, Buhongwa, Mwanza.

  • ••••••••••••••••••••••••••••••••

KILA la kheri kwa wagombeo wote wa uchaguzi wa TFF.

Amiri Msumi, Shungubweni.

  • ••••••••••••••••••••••••••••••••

POLENI Simba kwa kipigo kutoka kwa Orlando Pirates huko Sauz, kwani Okwi na Kichuya hawakucheza?

Juma Bundala, Iringa.

  • ••••••••••••••••••••••••••••••••

NAWASHANGAA mashabiki wa Yanga mnaofananisha kambi yetu ya Afrika Kusini sawa na yenu huko Morogoro, acheni kujidanganya mnachotakiwa kukubali kwa sasa kuwa mmefulia, maana mlidai mtaenda Zambia labda muende kwa ungo, subirini hukumu yenu Agosti 23.

Abdul, Dar.

  • ••••••••••••••••••••••••••••••••

NAMPONGEZA kiongozi wa kamati ya usajili ya Simba, Zakaria Hans Poppe kwani usajili huu ni bab kubwa tutaonana Agosti 23 na watani wetu Yanga kitaeleweka tu.

Mwanaid Khamis, Tabata, Dar.

  • ••••••••••••••••••••••••••••••••

WAZEE hao njaa zinawasumbua tu, kama wanazipenda timu kweli basi wasajili hata mchezaji mmoja tu.

Teketeke, Morogoro.

  • ••••••••••••••••••••••••••••••••

KWA Simba hii ya Mkude, Mzamiru, Kotei, Nyoni, Zimbwe, Kichuya, Niyonzima na Okwi nyie wazee wa 4G jiandaeni kula tano.

Ephrahim Manyama, Bugoji, Musoma.

  • ••••••••••••••••••••••••••••••••

NAIPONGEZA Yanga kwa kumruhusu Msuva kwenda Morocco, watani wetu kimyakimya sasa.

Magubo, Nyamagana, Mwanza.

  • ••••••••••••••••••••••••••••••••

KWA kweli Championi ndiyo habari ya mjini mnatoa habari nzuri sana na zinazoeleweka.

Athanas Charles, Morogoro.

  • ••••••••••••••••••••••••••••••••

SUALA la Mkude kupokonywa unahodha lisiwe ishu sana tumuachie kocha yeye ndiye anajua mipango yake.

Ashraf Kyamani, Arusha.

  • ••••••••••••••••••••••••••••••••

HONGERENI viongozi wa Simba kwa usajili mzuri, hawa wazee mbona sijawahi kuona wakihoji pesa za usajili zinatoka wapi.

Rafael Bilikwija, Tandika, Dar.

  • ••••••••••••••••••••••••••••••••

MKUDE usijali mabadiliko katika maisha ni kitu cha kawaida, kiroho safi jifunze kwa wakongwe akina John Bocco na Mwanjale. Simba ni taasisi, cha msingi ni nidhamu na uvumilivu kani bado una muda mrefu wa kuitumikia Simba. Kumbuka mambo mazuri hayataki haraka.

Kazimili, Kibaha, Pwani.

  • ••••••••••••••••••••••••••••••••

YANGA mpo, msihofu mashabiki wenzangu hao Simba hawatoki hiyo Agosti 23, subirini kuona kitakachotokea.

Christopher Mapunda, Kilombero, Morogoro.

  • ••••••••••••••••••••••••••••••••

CHONDECHONDE uongozi wetu wa Msimbazi mpeni Mohammed Dewji timu aiongoze.

Shedrack Matayo Irungu, Mashese, Mbeya.

  • ••••••••••••••••••••••••••••••••

NAPENDA kuzitakia maandalizi mema timu zote zitakazoshiriki ligi kuu msimu ujao.

Nehemia Msigala, Nanenane, Mbeya.

  • ••••••••••••••••••••••••••••••••

KAMA Nazareth ilifika mbali, Njombe Mji itashindwaje!

Joshua Makambako, Njombe.

  • ••••••••••••••••••••••••••••••••

NYIE Simba mnashangilia usajili sasa hivi baadaye mkija kufungwa na Kagera muende mahakamani tena.

Mustafa Nchimbi, Songea.

  • ••••••••••••••••••••••••••••••••

AZAM FC inatema wazee, wamatopeni wao wanawasajili, kweli kila mtu na akili zake.

Kibabu Maulid, Dar.

  • ••••••••••••••••••••••••••••••••

YANGA raha, usajili unafanywa kiufundi siyo kikosi cha mgambo mtaa wa pili.

Tumaini Francis, Mto wa Mbu.

  • ••••••••••••••••••••••••••••••••

HONGERA Aishi Manula kwa kujiunga na wenzako, Niyonzima nawe jiunge na wenzako ili kikosi kikamilike. Simba oyeee.

Peter Josiah, Shalemwa, Nzega.

  • ••••••••••••••••••••••••••••••••

MKUDE usiangalie kuvuliwa unahodha piga soka ili wajue uwezo wako, jitume mazoezini kwani Mungu yupo pamoja nawe ipo siku utacheza soka la kulipwa.

Frank Mgimba, Songea.

  • ••••••••••••••••••••••••••••••••

SIMBA kitu gani bwana, Yanga ndiyo habari ya mjini. Hapa Tshishimbi, Ngoma, Kamusoko yaani wamatopeni watakoma.

George Charles, Mirerani, Manyara.

  • ••••••••••••••••••••••••••••••••

HONGERA chama langu la Yanga kwa kuinasa saini ya kiungo mkabaji Papy Kabamba Tshishimbi, wamatopeni walie tu kwa kweli msimu huu.

Said Juma, Tandika, Dar.

  • ••••••••••••••••••••••••••••••••

HONGERA sana Simba kwa usajili mtamu lakini mnatambua asilimia 95 ya wachezaji wanaotoka Yanga hawajawahi kuwa watamu wakija Simba hata Niyonzima atachemka tu ila mtu akitoka Simba kwenda Yanga anakuwa tegemezi watazameni Dida, Barthez na Yondani.

Victor Wily, Dar.

  • ••••••••••••••••••••••••••••••••

NAIMANI kabisa kwa Okwi, Bocco na Niyonzima Yanga hawachomoki.

Pasco Deus, Sikonge, Tabora.

  • ••••••••••••••••••••••••••••••••

HONGERA chama langu Simba kwa usajili wenu yaani Bocco, Nyoni, Manula yeboyebo watatoka kweli?

Gidion Polepole, Ubaruku, Mbarali.

  • ••••••••••••••••••••••••••••••••

NAMPONGEZA Eric Shigongo kwa hadithi zake nzuri katika Championi, niko sambamba naye nafuatilia kila hadithi, kwani jamaa anatisha kama Simba.

Ditto Mwaipaja, Ipinda, Kyela.

  • ••••••••••••••••••••••••••••••••

ANAYEPINGA mabadiliko ndani ya Simba inabidi tumpime akili.

Shaban Mdamanyi, Kitunda Mayo, Tanga.

  • ••••••••••••••••••••••••••••••••

NIYONZIMA hapa Yanga wamepita Lunyamila, Ngassa na bado imebeba makombe.

Tyson Mniko, Tamau, Bunda.

  • ••••••••••••••••••••••••••••••••

Tuma Ujumbe wako kwa namba ya simu na Email hapa chini

Namba: +255 654 941010, Facebook: championigazeti Twitter:
championinewspaper E_mail: championiyetu2@Michezo na Burudani gmail.com

1 Comment
  1. […] na Championi Jumanne, John Bocco alisema ataanza kufungua akaunti yake ya mabao mbele ya Wanyarwanda hao baada […]

Leave A Reply