The House of Favourite Newspapers

John Bocco: Sasa Naanza Kazi Simba

0
Mshambuliaji mpya wa Simba, John Bocco ‘Adebayor’.

STRAIKA mpya wa Simba, John Bocco ‘Adebayor’ amebainisha bayana kuwa ataanza kuonyesha cheche zake za kutupia mabao ndani ya kikosi hicho kwenye mchezo wa Simba Day, leo Jumanne dhidi ya Rayon Sports ya Rwanda.

 

John Bocco aliyesajiliwa na Simba kwenye dirisha lililofungwa Jumapili iliyopita, leo Jumanne ataiongoza safu ya ushambuliaji ya Simba kwenye mchezo huo wa Simba Day dhidi ya mabingwa wa Rwanda, Rayon utakaopigwa Uwanja wa Taifa, Dar.

 

Akizungumza na Championi Jumanne, John Bocco alisema ataanza kufungua akaunti yake ya mabao mbele ya Wanyarwanda hao baada ya kushindwa kufanya hivyo kwenye mechi dhidi ya Bidvest Wits na Orlando Pirates, walizocheza nchini Afrika Kusini.

 

“Kwangu nimejiandaa vyema kwa ajili ya mchezo huo na niseme kuwa ndiyo itakuwa rasmi naanza kufungua akaunti yangu ya mabao baada ya kujiunga na timu hii.

 

“Na pia niwaambie wapenzi wa Simba, waje kwa wingi kuona kile ambacho nitakifanya kwenye mchezo huu wa Simba Day, kwani sitawaangusha hata kidogo na tuna uhakika mkubwa wa kushinda kwani tumejiandaa vyema kwa muda mrefu,” alisema mshambuliaji huyo.

Na: Said Ally | Championi

Leave A Reply