The House of Favourite Newspapers

Mbadala wa Herrera Pasua Kichwa Man U

Ander Herrera

KOCHA wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer amekiri kuwa timu yake ilifanya kosa kutosajili mbadala wa kiungo, Ander Herrera na uamuzi huo unaigharimu timu hiyo. Herrera aliondoka mwishoni mwa mismu uliopita baada ya kumaliza mkataba wa kuichezea Manchester United.

 

Kiungo huyo amejiunga na Paris St. Germain, ambayo ilifanikiwa kumchukua bure. Manchester United ilipoteza mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu England baada ya kufungwa nyumbani mabao 2-1 na Crystal Palace, wikiendi
iliyopita.

 

Kibaya zaidi ni kuwa Manchester United ilimuuza mapema pia kiungo wake mwingine, Marouane Fellaini. “Ninakiri kuwa tuna tatizo katika safu ya kiungo, tulipaswa kutafuta mbadala wa Herrera,” alisema Solskjaer, ambaye timu yake pia hivi karibuni ilitoka sare ya 1-1 na Wolves.

 

Solskjaer alisema kuwa Herrera alikuwa msaada mkubwa katika kutibua mipango ya timu pinzani wakati wa mechi. Alikiri kwa wachezaji wa kiungo waliopo katika kikosi chake wameshindwa kuvaa viatu vya Herrera. Alisema eneo la kiungo anatakiwa kufikiria namna ya kulitatua ili mambo yasizidi kuiharibikia timu hiyo.

Comments are closed.