The House of Favourite Newspapers
gunners X

Mbunge Mstaafu na Naibu Waziri Benedict Ole Nangoro Afariki Dunia

0

 

Aliyewahi kuwa Naibu Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi katika Serikali ya Awamu ya Nne, na Mbunge mstaafu wa Jimbo la Kiteto mkoani Manyara, Benedict Ole Nangoro.

Aliyewahi kuwa Naibu Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi katika Serikali ya Awamu ya Nne, na Mbunge mstaafu wa Jimbo la Kiteto mkoani Manyara, Benedict Ole Nangoro, amefariki dunia leo Desemba 7, 2025 akiwa anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mount Meru, Arusha.

Msemaji wa familia, Christopher Ole Sendeka, amesema Ole Nangoro alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya moyo, na aliwahi kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Benjamin Mkapa jijini Dodoma pamoja na hospitali nchini Kenya.

Amesema kwa sasa familia inaendelea na maandalizi, ikiwemo kupanga tarehe ya mazishi na eneo atakapozikwa.

MUFTI BAKWATA ATOA KAULI KUHUSU TEC na MAUAJI OKT 29 – ”NI HARAMU KUIUA NAFSI YA MTU BILA HAKI…”

Leave A Reply