Mhasibu Takukuru Atoroka, Atakayempata Kuzadiwa Mil 10 (Video)

Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru – PCCB), Brigedia Jenerali John Julius Mbungo.

 

NAIBU Mkurugenzi Mkuu  wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru – PCCB), Brigedia Jenerali John Julius Mbungo amesema  mfanyakazi mwenzao wa kitengo cha idara ya fedha,  Geofrey John Gugai, ametoroka kazini baada ya kutuhumiwa kumiliki mali nyingi tofauti na kipato chake.

 

Mbungo aliyesema hayo leo alipokutana waandishi wa habari na kusema kwamba Gugai ametoroka kazini baada ya mahojiano kati yake na ofisi yake kuhusu umiliki wa mali nyingi ambazo ni pamoja nyumba za kifahari na viwanja.

…Akiendelea kuongea na wanahabari.

Kiongozi huyo wa Takukuru alisema kwamba tuhuma dhidi ya Ndugai zilianza kutolewa na ofisi yake mwezi Mei mwaka huu kuhoji uhalali wa mali hizo ambapo baada ya kutoa ushirikiano wa muda na alipoonekana kukosa maelezo zaidi ya alivyozipata mali hizo, alitoroka kazini.

                                                                        Geofrey John Ndugai

Vilevile, amesisitiza kwamba mwananchi ambaye atatoa ushirikiano wa kuweza kumpata mtuhumiwa huyo, aitaarifu polisi au Takukuru ambapo atazawadiwa Sh.milioni 10 taslimu.

 

Kwa mujibu wa maelezo ya Mbungo, baadhi ya mali anazomiliki mtuhumiwa ni pamoja na nyumba ya ghorofa nne iliyopo Ununio; nyumba ya ghorofa tatu iliyopo Bunju; nyumba za kupangisha zilizopo Mbweni JKT zote zikiwa jijini Dar es Salaam.

 

Nyumba nyingine iko Majita, Musoma;  nyumba mbili zikiwa Kiseke na Nyegezi, Mwanza.

Zaidi ya nyumba hizo, anamiliki viwanja maeneo ya Bunju, Kigamboni, Mbuyuni-Temeke mkoani Dar es Salaam;  Bagamoyo, Kibaha mkoani Pwani;  huko Morogoro ana kiwanja huko Kihonda, Kiegea na Lukobe.

 

Viwanja vingine viko Kisasa, Itege na Kidachi mkoani  Dodoma;  vingine viko Nyegezi, Nyamanoro na Nyamagana mkoani Mwanza; ambapo ana viwanja vingine mikoa ya Musoma, Arusha, Tanga na kwengine.

(HABARI NA AMANI MADEBE NA DENIS MTIMA/GPL)

Kwa maelezo zaidi ya stori hii angalia video hii hapa chini:

Loading...

Stori zinazo husiana na ulizosoma

Toa comment