The House of Favourite Newspapers

MUNA: ULOKOLE SIYO KUJIBWETEKA

MWIGIZAJI wa Bongo Muvi ambaye kwa sasa amemrudia Mungu, Rose Alphonce ‘Muna’ amesema watu wengi wanafikiri mtu akiokoka, basi muda wote anashinda kanisani tu na siyo kufanya kitu kingine ambacho kinaweza kumsaidia kwenye maisha. 

 

Akizungumza na Za Motomoto, Muna ambaye sasa hivi amefungua duka la watoto la Patrick Classic kwa ajili ya kumuenzi marehemu mwanaye Patrick, alisema watu wengi wakiona mtu unajishughulisha na biashara wanaanza madongo kuwa umeacha ulokole.

 

“Unajua hakuna jema unaweza kufanya kwa mtu akakuelewa kabisa na wengi wanapenda kukuona unashinda kanisani ndiyo waamini kuwa wewe mlokole, kumbe wanatafisiri tofauti kabisa kwa sababu kila mmoja anapaswa kufanya kazi,” alisema Muna.

Comments are closed.