The House of Favourite Newspapers

Ndemla: Nipo tayari kusaini Yanga FC

KIUNGO wa Simba, Said Ndemla, ametoa msimamo wake akisema kuwa hana haraka ya kusaini klabuni hapo kwa kuwa anataka kucheza nje ya nchi, lakini akasisitiza ikishindikana nje hata Yanga yupo tayari kusaini.

 

Katika msimu huu, Ndemla alipewa ruhusa na Simba ya kwenda kufanya majaribio katika timu ya Eskilstuna ya Sweden, ambapo hadi sasa majibu yake kama alifuzu au la yalibaki kuwa kitendawili.

Akizungumza na Championi Jumatatu juzi, Ndemla alisema pamoja na mkataba wake kufikia ukingoni mwishoni mwa msimu huu, hana haraka ya kuongeza mpya, hadi hapo dili lake la kwenda kucheza nje ya nchi litakaposhindikana.

 

“Sina mpango wa kusaini Simba mapema hii, zaidi najipanga kuangalia dili langu la kucheza nje ya nchi, endapo nitakwama basi nitakuwa tayari kusaini Yanga au kuongeza mkataba Simba kama watakuwa bado wanahitaji huduma yangu.

 

“Tetesi zote ambazo zimekuwa zikisemwa juu yangu naweza kusema zitabaki kuwa tetesi ila mipango kamili naijua mwenyewe, japo nasikia kuna watu wanazusha eti kuwa nilitolewa kambini kisa niligoma kusaini Simba, hilo si kweli, mimi ninaumwa sasa ni wiki nipo tu nyumbani naendelea na matibabu,” alisema Ndemla.

 

WILBERT MOLANDI, Dar es Salaam

Comments are closed.