visa

 PENZI LA KIBA LAMTESA MREMBO!

TOA la moyoni! Ndivyo unavyoweza kusema kufuatia mrembo mmoja anayetumia jina la Nancy_The_Beuty kueleza hisia zake za mapenzi kwa staa wa Bongo Fleva, Ali Saleh Kiba ‘Alikiba’.  Kupitia ukurasa wake huo, mrembo huyo alitiririka maneno kwamba, anamkubali sana Alikiba na ikiwezekana ahamishie majeshi kwake.

“Nimeficha hisia zangu kwa muda mrefu, nimejitahidi kunyamaza lakini naona nashindwa acha tu niweke wazi… Alikiba, silali kwa ajili yako! Najua umeoa ila nashindwa nifanyeje wakati kuu-control moyo siwezi…” alandika mrembo huyo. Baada ya kuandika hivyo, wapo waliompongeza kwa kueleza hisia zake lakini wengine walimponda kwa kusema anatafuta kiki!
Toa comment