SANCHI ANAANGALIA MAHABA ZAIDI

Modo mwenye jina kubwa ndani na nje ya Bongo, Jane Rimoy ‘Sanchi’ ameweka wazi kuwa, mwanaume ambaye atamuoa haangalii anatoa mahari kiasi gani, bali anaangalia mahaba yake. Akizungumza na Gazeti la Ijumaa Wikienda, Sanchi alisema wengi wanadhani kulipiwa mahari kubwa ni ufahari, lakini wanapoingia kwenye ndoa wanakutana na mambo ambayo hawawezi kuyahimili hivyo kuachika.

“Mama yangu amenifundisha vizuri sana kuwa nisione mtu anataka kuniposa kwa mamilioni nikajua ndiyo nimepata, bora hata mtu atoe elfu hamsini, lakini akawa yupo vizuri kwenye mahaba,” alisema Sanchi.


Loading...

Toa comment