The House of Favourite Newspapers

Sanchoka: ‘Nilimuokota’ Idris Sultan Kwenye Apartment Sauzi, Amfungukia Gigy Money

sanchoka-1      

MODO mwenye figa la kuvutia anayekuja kwa kasi kwenye tasnia ya urembo, Sanchoka yeye hupenda kujiita Sanchi ameanika namna ambavyo alikutana na anayedaiwa kuwa mpenzi wake kwa sasa, Mshindi wa Big Brother Africa 2014 na mtangazaji wa Choice FM, Idris Sultan.

sanchoka-7Akifanya mahojiano (Exclusive Interview) na Channel maarufu hapa mjini ya Global TV Online, Sanchoka amefunguka kuwa uhusiano wake na Idris ulianzia kwenye Apartment wakati walipokuwa wamekwenda Afrika Kusini (Sauzi) kushuhudia utoaji wa Tuzo za MTV Africa (Mama) hivi karibuni.

“Mimi na rafiki zangu tulipanga kwenda kushuhudia MTV Awards huko Sauzi, bahati mbaya apartment tuliyofikia ndipo alipokuwa amefikia Idris pia.”

sanchoka-2-1024x1024

“Tulikuwa watu wengi kwenye hiyo apartment, walikuwepo wakina Shilole, na wengine wengi,”

Akanusha kuhusu kuwa wapenzi

Licha ya kuelezea kinagaubaga alivyokutana na Idris, Sanchoka amekanusha kuhusu taarifa zinazosambaa kuwa ana uhusiano wa kimapenzi na mshindi huyo wa BBA 2014.

“Idris alikuwa ana-anounce (anatangaza) awards, kwa kuwa alikuwa VIP kule mbele, alinifuata na kuniomba niwe partner wake ili twende nikakae naye kule mbele, haikuwa urafiki wa mapenzi bali ulikuwa urafiki wa kawaida tu.” Ameeleza Sanchoka ndani ya Studio za Global TV.

idrissultanIdir Sultan.

Amfungukia Gigy Money

Mbali na kufunguka alivyokutana na Idris, Sauz amefunguka pia kuhusu uhusiano wake na modo mwenzake ambaye pia ni mtangazaji wa Choice FM, Gigy Money ambaye alidaiwa kutoka kimapenzi na Idris huyo huyo.

sanchoka-8“Uhusiano wao (Idris na Gigy) mimi haujani-affect chochote kwa kuwa mimi na Idris tulikuwa marafiki wa kawaida tu, na hatujawahi kuzungumzia kuwa na uhusiano wa kimapenzi”. Alisema Sanchoka.

gigy na idris (2)Idris na Gigy Money

Pia Sanchoka ameeleza kuwa yeye kwa sasa ana mchumba wake mbali na huyo wanayemsema mitandaoni (Idris), licha ya kutobainisha iwapo atafanya taratibu za kufunga naye ndoa siku za hivi karibuni.

Idris aishia ‘Kula Kwa Macho’ Kwa Sanchoka

rap

Mabusu ya Jokate kwa Kiba Baada ya Kupiga Hatrick Tuzo za EATV 2016

Comments are closed.