The House of Favourite Newspapers

Serikali Yatoa Ndege kwa Yanga Kuwapeleka Katika Mchezo wa Fainali

0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameahidi kutoa Tsh milioni 20 ikiwa klabu ya Yanga itaibuka na ushindi kwenye fainali ya kombe la Shirikisho Afrika na amesema Serikali itatoa ndege itakayowabeba wachezaji na mashabiki wa Yanga kwenda kwenye mchezo wa fainali

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa minara 21 ya kurushia matangazo ya televisheni ardhini (DTT) ya kampuni ya Azam Media Dkt Samia amesema:-

“Nilianza na Milioni 5 kwa kila goli la ushindi , waliposogea nikaweka Milioni 10 kwa kila goli la ushindi, tunapokwenda kwenye Fainali ni Milioni 20 timu ikitoka na Ushindi ”

“Milioni 20 hizi hazitakwenda akifungwa 2 au 1 hapana! yawe magoli yote ambayo yameipa timu ushindi kila goli Milioni 20 ”

“Serikali itatoa ndege kuwapeleka katika mchezo wa Fainali , Ndege hiyo itabeba Wachezaji na Mashabiki. Ndege hii itawapeleka , itawasubiri na kuwarudisha Nchini ”

Leave A Reply