Simba kukabidhiwa leo kombe lao Uwanja wa Taifa – Video

MCHEZO wa leo wa Ligi Kuu Bara kati ya Simba dhidi ya Biashara United Uwanja wa Taifa, Dar umepangwa kuanza kuchezwa saa tisa alasiri ili kupisha shamrashamra za ubingwa na kukabidhiwa taji la Ligi Kuu Bara msimu wa 2018/19 kwa mabingwa hao.

 

Simba ilitangaza ubingwa wake huo katika mchezo uliopita wa ligi dhidi ya Singida United uliopigwa kwenye Uwanja wa Namfua, Singida kwa mabingwa hao kushinda mabao 2-0.

 

Timu hiyo baada ya ushindi huo ilifi kisha pointi 91 ambazo hazitafi kiwa timu yoyote wakiwemo watani wao wa jadi, Yanga walio na pointi 86 wakiwa wamebakisha mchezo mmoja pekee.

 

Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Championi Jumamosi na kuthibitishwa na Meneja Mkuu wa Simba, Patrick Wilbert Rweyemamu, mchezo hautapigwa tena saa kumi jioni na badala yake saa tisa alasiri. Rweyemamu alisema wamepokea taarifa za kurudishwa saa nyuma za mchezo huo ili kupisha shamrashamra za ubingwa huo pamoja na kukabidhi kombe lao.

“Mchezo wetu wa kesho dhidi ya Biashara utaanza saa tisa kamili alasiri kwenye Uwanja wa Taifa, Dar kwa sababu baada ya mchezo huo kutakuwa na makabidhiano ya ubingwa wa ligi.

 

“Katika makabidhiano hayo, kutakuwa na shamrashamra za wachezaji, viongozi na mashabiki za ubingwa baada ya kuchukua kwa mara ya pili mfululizo kombe hilo,” alisema Rweyemamu.

 

Hata hivyo katika mchezo huo ambao Simba itakabidhiwa ubingwa mgeni rasmi atakuwa ni Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola. Msimu uliopita Simba walikabidhiwa kombe na Rais wa nchi John Pombe Magufuli.

HAJI MANARA Atoa Taarifa SIMBA Watakavyopokea Kombe kwa Msafara

Loading...

Toa comment