The House of Favourite Newspapers

Simba Queens yalipa kisasi kwa Baobab

TIMU ya Simba Queens imeendelea kuonyesha ubabe kwenye Ligi Kuu ya Wanawake ya Serengeti Lite, baada ya kuiadhibu timu ya Baobab mabao 6-0 kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar, juzi.

 

Mabao ya Simba yalifungwa Jackline Albert aliyefunga matatu ‘Hat Trick’ huku mengine yakifungwa na Opah Sanga aliyefunga mawili pamoja na Joel Bukuru aliyefunga moja kwa penalti.

 

Simba katika mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo walifungwa na timu ya Baobab mabao 3-1 kwenye Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.

 

Simba Queens wapo nafasi ya pili wakiwa na pointi 38, anayeongoza msimamo huo ni JKT Queens wenye pointi 57 ambao wameshatwaa ubingwa.

MARCO MZUMBE, Dar es Salaam

HAPATOSHI BUNGENI: Waziri KIGWANGALA Abanwa, Chanzo cha Migogoro!

Comments are closed.