The House of Favourite Newspapers

TAJIRI BONGO AJIUA KWA RISASI

George Ndendya enzi za uhai wake.

 

MFANYABIASHARA ambaye ni tajiri maarufu mjini Mafinga wilayani Mufindi, Iringa, George Ndendya (50), anadaiwa kujiua kwa kujipiga risasi kwa kile kilichosemekana kuwa ni kukwepa kudhalilishwa kutokana na deni analodaiwa na benki (jina linahifadhiwa).

Katika mahojiano na Ijumaa baada ya kujiri kwa tukio hilo lililojaa simanzi Machi 9, mwaka huu mjini Mafinga, mke wa marehemu, Lucy Ndendya alisema kuwa, kabla ya kujiua kwa kujipiga risasi, mumewe huyo aliacha ujumbe juu ya sababu ya kuamua kujitoa uhai.

 

AVAMIWA, APORWA MIL. 15

Lucy alisema kuwa, siku chache kabla ya tukio hilo, mumewe alivamiwa na majambazi katika eneo la Kinengembasi alipokuwa akitokea safarini huko Makambako mkoani Njombe na kuporwa pesa taslimu zaidi ya shilingi milioni 15.

“Alipovamiwa, aliwekewa dawa za kulevya kisha akawa amezimia hivyo ilibidi apelekwe hospitalini. Baada ya matibabu alirejea mjini Mafinga akiwa amepona kabisa.

 

George Ndendya enzi za uhai wake.

AENDA DAR KUFUATA MBOLEA

“Baada ya kupona, alikwenda jijini Dar kufuata mbolea.  Alipokuwa safarini kurejea Iringa alifi ka Morogoro akawa amazidiwa na kulazwa tena,” alisema mwanamama huyo.

Mjane huyo alisema kuwa, baada ya kutoka mkoani Morogoro, akiwa anaendelea vizuri, aliwasiliana naye kwa njia ya simu na kumueleza kwamba alifi ka salama mjini Mafinga.

“Wakati nikiwasiliana naye nilikuwa njiani nikitokea Njombe kushiriki mazishi. Nilipofi ka nyumbani nilikuta mlango umefungwa kwa ndani.

 

AONA MWILI WA MUMEWE NDANI

“Niligonga sana mlango, lakini ulikuwa haufunguliwi. Nilimuuliza kijana wangu wa dukani kuwa mbona mlango umefungwa kwa ndani?

“Aliniambia baba yupo ndani. Nilipompigia simu, iliita bila kupokelewa.

“Nilipochungulia kwa dirishani, nilimuona mume wangu amelala chini huku kukiwa na damu.

“Nilishtuka sana na kutaharuki, sikuweza kufanya chochote zaidi ya kumfuata balozi wa nyumba kumi ambaye nilikuja naye kisha tukavunja mlango.

Mke wa Marehemu.

 

UJUMBE MZITO

“Tulipoingia ndani, sikuamini macho yangu. Mume wangu alikuwa amejiua kwa kujipiga risasi…roho inaumaa…(kilio),” alisimulia Lucy kwa majonzi makubwa huku akionesha sehemu ya ujumbe mzito alioacha mumewe uliosomeka:

“Nimedhalilishwa vya kutosha kiasi kwamba sitaweza kufanya biashara yoyote kwa sasa.

Ahsante, George Lucas Ndendya… Dickson Mwani ataleta mbolea CAN 600 na UREA Zakaria pokea, ukiona amechelewa mpigie simu, nadhani unamfahamu. Mimi nimeamua kurudi hapa nyumbani kwa ajili ya hili.”

 

RAFIKI ASIMULIA SIKU YA TUKIO

Kwa upande wake, rafiki mkubwa na mshauri wa kibiashara wa marehemu huyo, George Chaula alisema kuwa, siku ya tukio, kabla ya kujiua kwa mfanyabiashara huyo tajiri alimpigia simu kumtaka afike nyumbani kwake ili afanye naye mazungumzo.

“Aliponipigia simu, aliniomba tukutane asubuhi. Nilipofi ka dukani kwake, kijana wake aliniambia kuwa jamaa alisema mtu wa kwanza kuongea naye awe ni mimi na asiingie mtu mwingine ndani kwake.

“Nilipojaribu kumpigia simu alikuwa hapatikani ndipo nilipoamua kwenda stendi kumsindikiza mke wangu kwanza,” alisema Chaula.

Kamanda wa Polisi Mkoa (RPC) wa Iringa, ACP Juma Bwire.

 

Chaula alisema kuwa, baada ya kufi ka stendi, ghafla alipigiwa simu na mjane wa marehemu akilia na kumtaka akimbilie nyumbani kwake na baada ya kufi ka alimkuta jamaa ameshajiua.

DENI MILIONI 80

Hata hivyo, alisema kuwa, kabla ya kujiua kwake, siku kumi za nyuma, pamoja na kuvamiwa na majambazi na kuporwa pesa kiasi kikubwa cha pesa, nyumba zake mbili zilikuwa zikinadiwa na moja ya benki wilayani Mufindi na alikuwa akidaiwa takribani shilingi milioni 80.

 

RPC ATHIBITISHA

Kamanda wa Polisi Mkoa (RPC) wa Iringa, ACP Juma Bwire alithibitisha kutokea kwa kifo cha mfanyabiashara huyo na kusema kuwa alikuwa akiishi nyumba Block J Changarawe mjini Mafinga Wilaya ya Mufindi.

 

Kamanda Bwire alikiri kuwa, mfanyabiashara huyo alijipiga risasi kwenye paji la uso kwa bastola aina ya Star Browes yenye namba za usajili A438803 aliyokuwa akiimiliki kihalali. Alisema kuwa, chanzo cha kujiua ni msongo kutokana na ujumbe alioandika mwenyewe kabla ya kujiua.

 

MAZISHI

Mazishi ya mfanyabiashara huyo yalifanyika wiki iliyopita mjini Mafi nga na kuhudhuriwa na umati mkubwa wa kada mbalimbali kutokana na kuwa na jina kubwa alilolipata kupitia biashara zake hasa za mbolea na mazao.

STORI: FRANCIS GODWIN, IRINGA.

 

BABU MBARONI KWA KUGUSHI VYETI, AKUTWA NA MIHURI 54 YA MAGUMASHI

Comments are closed.