The House of Favourite Newspapers

Vieira: AFCON Inastahili Heshima Zaidi

0

Meneja wa klabu ya Crystal Palace, Patrick Vieira amesema kuwa michuano ya AFCON inastahili heshima zaidi.
Vieira anategemea kupoteza wachezaji wake watatu michuano hiyo itakapoanza mnamo Januari 9.

 

Wachezaji hao ni Cheikhou Kouyate (Senegal) Wilfried Zaha (Ivory Coast) na Jordan Ayew (Ghana).

“Ninaheshimu na kuelewa umuhimu wa wachezaji kwenda kuziwakilisha nchi zao. Hivyo kamwe siwezi kumzuia mchezaji kwenda kwenye AFCON. Ninaamini AFCON inatakiwa kuheshimiwa, maana ina umuhimu sawa na ule wa UEFA,” amesema Vieira.

Aidha, Vieira amewataka waandishi wa habari kutoka ulaya kufuatilia AFCON kwa karibu zaidi na kuripoti matukio muhimu.

Leave A Reply