×

Washindi wa Tuzo za TMA Kupata Bima ya Afya, Pensheni-Mchengerwa

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo,  Mohamed Mchengerwa

WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa na Michezo,  Mohamed Mchengerwa kwenye utoaji wa Tuzo za Muziki Tanzania (TMA)  Aprili 02, 2022 amesema kuwa washindi wote wa tuzo za hizo watafunguliwa Bima za Afya na Pensheni kwa muda wa mwaka mmoja zitakazo wasaidia katika kazi zao muziki.

“Tumeamua kufanya hivi katika tuzo hizi ili kuwapa thamani wanamuziki, lakini pia Bima hizi zitawasaidia katika kazi zao na hata Pensheni zitawasaidia pale watakapokuwa wazee, tumetoa kwa mwaka mmoja lakini baada ya hapo wanaweza kuendeleza wenyewe,” Waziri Mchengerwa.

Leave a Comment